Elections 2010 No One KiCKS a dead dog

kingwipa1

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2008
Posts
334
Reaction score
51
Tangu kuanza kwa kampeni za ubunge na urais tumeshuhudia majibizano mengi ya maneno na kuchafuana kunakolenga kupunguza nguvu ya upande mmoja. Katika kuchunguza kwangu nimegundua kuwa walengwa wakubwa wa kushambuliwa ni Kikwete na Dr. Slaa. Kikwete anashambuliwa kwa kuwa anagombea huku akiwa na kofia ya urais. Dr. Slaa anashambuliwa kwa kuwa ni mgombea wa upinzani mwenye mvuto mkubwa miongoni wa mwa wananchi na tangu kutangaza kwake kugombea kiti cha urais amekuwa gumzo kubwa ndani na nje ya nchi.

Ninachojua mimi "No One kicks a dead dog", ukiona Slaa anashambuliwa kwa nguvu na wana CCM ni picha wazi kuwa amewatikisa kiasi cha kushindwa kutulia kwenye viti vyao. Hakuna mwana CCM aliyetegemea kuwa mtaji wao (Kikwete) atapata pingamizi kubwa katika mbio zake za kuwania urais mwaka 2010.

Swali ni kwa nini hatusikii habari za wagombea wengine kama Lipumba (CUF) ambaye amewahi kuwa maarufu?

Always remember, no one shoots at a dead dog!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…