Hivi mradi wa mafuta wa Lokichar uliishia wapi?
Nakumbuka ulifunguliwa kwa hamasa sana na kipindi kile ndio ulikua hot topic humu, maendeleo yake so far?
Kenya wana miradi mizuri sana ila sijui wanafeli wapi, nafikiri hii miradi haifanyiwi feasibility studies za maana ndio maana mradi kama wa LAPSSET unajengwa mwaka wa 10 sasa na bado hata 40% hujafika, sitaki kuongelea kuhusu SGR to Malaba ambao na wenyewe umeshakufa rasmi.
Mradi wa JKIA to CBD electric commuter train uliokua ufadhiliwe na Macron na wenyewe umebaki story, the list is endless and rampant, inasikitisha.