the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 395
- 570
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayehusika na Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, amewataka Watanzania kupuuza madai ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwamba uchaguzi hautafanyika bila mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi.
Akizungumza siku ya Jumanne Machi 4, 2025 katika kikao cha viongozi wa CCM wa mashina, kata, matawi na mabalozi wa Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Makalla amesema kuwa CHADEMA inakosea kuwaambia wafuasi wao wasijiandikishe kwa madai kuwa hakutakuwa na uchaguzi.
"CHADEMA wameshawaambia wafuasi wao wasijiandikishe kwa sababu hakutakuwa na uchaguzi, kwa hiyo wameanza kushindwa kabla. Wanajiongezea matatizo kwa kukosa wanachama wao kujiandikisha. Nilimsikia Tundu Lissu akisema ‘Ujiandikishe iweje? So what?’ Nikasema shughuli imeisha hapa, hawa wameshakubali kushindwa," amesema Makalla.
Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Ameendelea kusisitiza kuwa uchaguzi utafanyika kwa mujibu wa sheria na katiba, na kwamba madai ya CHADEMA kwamba "No Reform, No Election" ni propaganda zisizo na msingi.
"Reform zimeshafanyika na uchaguzi utafanyika. Ninataka niseme ukweli, puuzeni propaganda kwamba eti ‘No Reform, No Election’. Uchaguzi upo. CHADEMA hawana mamlaka wala uwezo wa kuzuia uchaguzi, wanapoteza muda wao na wa Watanzania. Uchaguzi upo kwa mujibu wa sheria na katiba, na hakuna chama chochote kinachoweza kuuzuia," amesisitiza Makalla.
Kauli yake inakuja huku mijadala ikiendelea kuhusu mustakabali wa uchaguzi na msimamo wa vyama vya siasa juu ya mazingira ya kisiasa nchini Tanzania.
Source: Jambo TV