The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
View: https://youtu.be/ANA3rytxn0Q?si=6caBpBCIieREJQl7
➡Ukimtazama na kumsikiliza vizuri Ansbert Ngurumo ktk video hii unaweza kudhani ni mtu neutral, anayejaribu kushauri pande mbili ili kurekebisha mambo yao. Lakini ukweli ni kuwa, anajaribu kutumia ujuzi na usomi wake wa kihabari kupunguza makali ya kaulimbiu ya CHADEMA ya NO REFORMS, NO ELECTION ktk namna ya kuwa - confuse ambao tayari wameshaielewa na wako tayari kuitekeleza kwa vitendo...
➡Ukimtazama na kumsikiliza kwa makini utagundua kuwa, huyu bwana anauchukia kupindukia uongozi mpya wa CHADEMA chini ya Mwenyekiti mpya Tundu Lissu. Sikiliza kauli zake kwenye video hii...
➡Huyu bila shaka alikuwa ni mmoja wa chawa wa Freeman Mbowe aliyeshindwa. Na bado mpaka sasa haamini kuwa boss wake alishindwa na sio Mwenyekiti tena..!
##Hivi kwa akili za kawaida tu, mtu yeyote anaweza kujiuliza maswali haya:
1. Hivi ni kweli Ansbert Ngurumo haelewi mantiki ya kauli mbiu hii ya NO REFORMS, NO ELECTION..?
2. Hivi ni kweli Ansbert Ngurumo hajui kuwa kilele cha mfumo mbovu na mbaya kabisa wa uchaguzi Tanzania umethibitishwa na chaguzi za mwaka 2019, 2020 na 2024...?
#Anyway, hebu mtazame na msikilize hadi mwisho kisha, na wewe sema neno..