Mla Bata
JF-Expert Member
- Jan 24, 2013
- 7,841
- 17,491
No shave November,
Nini maana yake?
Dunia ina mengi....
Hiki ni kipindi cha mwezi mmoja wa kumi na moja ambapo wanaume huweka utaratibu wa kuachia/ kutokunyoa ndevu zao kwaajili ya la kusave gharama ya kunyoa kwa lengo la kutumia fedha hizo kuchangia gharama za matibabu ya wagonjwa wa kansa duniani, pia kuongeza uelewa juu ya ugonjwa huo hatari kwa sasa duniani.
Asili yake.
Harakati hizi zilianzia kwenye mitandao ya kijamii hasa facebook huko nchini Marekani mnamo mwaka 2009 lakini ilipofika mwaka 2013 harakati hizi zilipata nguvu baada ya American Cancer Society kutambua harakati hizi na kuanza kuunga mkono Hii haikuwa mara ya kwanza kwa harakati kama hizi
Nchini Australia [emoji1037] mwishoni mwa miaka ya tisini kulikuwapo na harakati kama hizi ambapo nchini humo kulihusisha ufugaji wa mustaches "sharubu" kwa vijana wengi lengo likiwa ni hilo hilo moja huku movement hizo zikiitwa MOVEMBER , ikiwa na maana ya Moustache November.
Kutokana na utandawazi na kukua kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii harakati hizi zimeenea nchi nyingi kwa vijana na wanaume wa makamo kujiunga na harakati hizi, huku wengine wakifanya kama mitindo, "fashion".
Kwa nchi za wenzetu hasa Marekani , wameenda mbali zaidi kutokana na harakati hizi kuwa serious na zinazotambulika huku kukiwa na utaratibu maalumu wa kuchangia pesa kwaajili ya gharama za matibabu na kuongeza ufahamu juu ya ugonjwa huo.
Ni mwezi wa kumi lakini kwa wenzangu na mimi ambao tumekuwa na utaratibu huu , huu ndio muda muafaka wa kuanza kuachia "MIJIDEVU" yetu [emoji3] kuelekea November.