No smoking

No smoking

Joined
Nov 11, 2008
Posts
782
Reaction score
40
TANZANIA.
Baada ya kupitishwa sheria ya kuzuia uvutaji sigara migahawani na hotelini,
Serikali iliamuru kila wenye migahawa au hoteli kuweka tangazo la sheria hiyo,
mambo yalikwenda kama ufuatavyo:

MATANGAZO:

Mgahawa wa Msomali: Habana kufuta dumbago habah,
kama nafuta dumbago haba serkali atashkuwa hatwa mkali
kabeisa.

Mwarabu: Habana kufuta mtumbatu ndani ya myumba hii, mtu ukufuta
mtumbatu haba tabigwa kwa kishwa yake halafu tabelekwa kwa bolis!

Jaluo....... Ni makufuru kuvuta singara kipande ii. Kama we nakamatwa
inavuta singara kipande iii tapelekwa direct kwa prison.


Mhindi....Serkali sema pana buta sigara apa. basi watu ote pana buta sigara apa!


Makonde; Hailuuchiwi kubuta chigala apa otelini. Ukibuta chigala apa utapigwa nchale na kupelekwa chelikalini!

Msukuma: Inakatazwagwa kuvutaga masigala apa. mtu akivunja hili lishelia
atapelekwa kwa mwanagwa jitabu.

Mpemba. Sigara zeshakatazwa kuvutiwa humu ngahawani hivo, na msifanye nchezo, Bwan Juma ni nkali atawatia jela wabishao na atawatoa kwenye CUF!

Hoteli ya mwana CCM:
Kufatana na sababu zisizoweza kuzuilika, serikali imechukuwa hatua nyeti ya
kupinga uvutaji wa sigara kidamnasi ya watu, migahawani na mahotelini. Pia imeelezwa kinagaubwaga kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka sheria hii. Wahudumiwa wote wanapaswa kuzingatia amri hii
ili kuepukana na kile kinachojulikana kama mkono wa sheria.
 
jamani..... sipati picha ikiwa kwenye audio..

.......ila huyo mpemba yuuko juUUUU.
 
Back
Top Bottom