Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Mbona unaongea kana kwamba hujui kuwa walicho nacho huko majuu ni mkusanyiko wa siku nyingi (cumulative effect) wa wataalam na utaalam ambao sisi 'miafrika ndivyo tulivyo' tumechangia kwa kiasi kikubwa toka enzi za utumwa, ukoloni na ufisadi wa maarifa yetu kwenye vyuo vyetu vya kale kama Timbuktu na Alexandria. Majuu imetegemea sana watu wenye asili ya Afrika kwa miaka mingi sana. Huyu, je, unamjua - aliwasaidia sana kutengeneza Modeli za Uchumi mpaka wakampa U-Sir:
Mchango wetu sisi Miafrika kwa kiasi kikubwa sana ni kazi za kutumia miguvu. Tokea utumwani hadi kwenye ukoloni.
Na kama tungekuwa wataalam hivyo basi tungewastukia wazungu tokea mwanzo na kuwapiga chini. Tungewageuzia kibao.
Na hivyo so called vyuo vya Timbuktu na Alexandria leo hii vinafanya nini? Maana mara ya mwisho kuona Timbuktu kwenye Tivii niliona kuwa ni sehemu iliyochoka sana. Hakuna lolote huko. Ni jangwa, mivumbi, mchanga, na jua kali tu. Nenda Oxford uone jinsi palivyo....