Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
NOAH SAPUTU MOLLEL - ASISITIZA USAWA KATIKA AJIRA ZINAZOTANGAZWA TAMISEMI
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi Mhe. Noah Lemburis Saputu Mollel wakati akichangia bungeni katika vikao vinavyoendelea amesisitiza pawepo na usawa katika kugawa ajira pia ameiomba Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuwa barabara za Arumeru zitengenezwe.
"Barabara ya Loning'o kwenda Mringa imekatika daraja, Barabara kutoka mnadani kwenda hospitali ya Oturumenti imekatika, naiomba sana wizara kupitia waziri wetu aone namna gani tunapata fedha za dharura, kwa ajili ya kuhakikisha maeneo haya yaliyokatika yanaweza kutengenezwa mara moja"Noah Lemburis Saputu Mollel -Mbunge wa Arumeru Magharibi.
"Nina meseji zaidi ya 200 mpaka 300 vijana wanasema tutafutieni ajira, kwa hiyo niombe basi ajira hzi zigawanywe kwa mikoa, na baadae kwenye mikoa igawanywe kwenye Wilaya ili tuweze kupata usawa katika kupata ajira hizi"Noah Lemburis Saputu Mollel -Mbunge wa Arumeru Magharibi.