Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
MANCHESTER, ENGLAND
ASIKWAMBIE mtu, ukiwa na pesa kila mtu anataka kuja kufanya kazi kwako. Si anajua utamlipa vizuri?
Basi hilo ndilo linalotokea huko Manchester United. Kuna makocha sita wamewekwa kwenye orodha na wanachuana kwelikweli kila mmoja akiamini ana vigezo vinavyofaa kuchukua mikoba ya kuinoa timu hiyo yenye maskani yake Old Trafford.
Si unajua Man United kwa sasa inanolewa na kocha wa muda tu, Ole Gunnar Solskjaer. Ikifika mwishoni mwa msimu itahitaji kuwa na kocha wa kudumu kuchukua mikoba iliyoachwa na Jose Mourinho aliyefutwa kazi mwezi uliopita.
Unaambiwa hivi, Makamu Mwenyekiti wa Man United, Ed Woodward kwa sasa yupo kwenye wakati mgumu kwelikweli katika kumpata kocha ambaye ataweza kudumisha utamaduni wa timu hiyo ikiwamo kuifanya akademia kuwa na nguvu pamoja na kuwatumia makinda watakaohitimu kutoka kwenye shule yao ya soka.
Kwa sasa kazi ya kuinoa Man United inafanywa na Kocha Solsjkaer. Kitu kinachofanya kila kocha atake kuinoa Man United ni utajiri wa klabu hiyo. Kwanza inalipa mshahara wa kibosi na pili, sio bahari, inatoa mkwanja wa kusajili inapohitajika kufanya hivyo, tena inasajili kwa pesa yoyote ile, ilimradi tu mchezaji mwenyewe awe kwenye mipango ya kocha wake.
Makocha David Moyes, Louis van Gaal na Mourinho wote waliopita kwenye timu hiyo baada ya kuondoka Sir Alex Ferguson walipewa nafasi ya kusajili wachezaji waliowataka, tena kwa bei kubwa. Moyes alimsajili Juan Mata kwa pesa ndefu, Van Gaal alimsajili Angel Di Maria kwa mkwanja wa maana na Mourinho alimsajili Paul Pogba kwa pesa iliyovunja rekodi ya dunia kwa wakati fulani.
Kwenye orodha hiyo ya makocha sita, mmoja wao ni Solskjaer. Bahati ya kocha huyo, ambaye ni staa wa zamani wa Man United ni kwamba amepewa kazi kwa muda na huu ni wakati wake wa kuonyesha kweli anastahili kupewa mkataba wa moja kwa moja.
Solskjaer ameanza kuzikonga nyoyo za mashabiki wa timu hiyo hasa baada ya kuonyesha ni mpenzi wa soka la kushambulia ambalo limewafanya wachezaji Pogba, Marcus Rashford na Anthony Martial kuonyesha ubora mkubwa sana ndani ya uwanja. Katika mechi tatu zilizopita kabla ya mechi ya usiku wa jana, Man United ilifunga mabao 12.
Kutokana na mwanzo huo bora kabisa, Solsjkaer sasa naye yupo kwenye nafasi kubwa ya kukamatia kibarua hicho cha kudumu, kwa mujibu ya taarifa zinazoelezwa.
Majina ya makocha wengine waliopo kwenye mchakato wa kuitaka kazi hiyo iliyomshinda Mourinho ni Mauricio Pochettino wa Tottenham Hotspur, ambaye jina lake limekuwa likitajwa tangu Special One alipofutwa kazi. Taarifa zinadai Man United ilimtaka Pochettino tangu mwaka 2016, lakini akagoma kwenda Old Trafford na kubaki zake kwenye kikosi cha Spurs.
Safari hii Man United imetangaza vita kuwa italipa pesa inayotakiwa na Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy ili kumnasa Pochettino, lakini Spurs imekuwa akiweka ngumu kwa sababu inataka ihamie kwenye uwanja wake mpya ikiwa na kocha bora kabisa kwenye benchi lake.
Kocha mwingine, anayehusishwa na kibarua hicho jina lake likitajwa sana ni Zinedine Zidane.
Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid CV yake iko vizuri na jambo zuri kwa sasa hana kazi, hivyo kumpata kwake huhitaji kutoa pesa kama ilivyo kwa Pochettino.
Kulikuwa na taarifa Zidane alikutana na balozi wa Man United huko Dubai na kuzidisha uvumi kuwa moja ya mambo yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye mazungumzo ni kuhusu kutua Old Trafford.
Laurent Blanc, aliyewahi kuichezea Man United naye yupo kwenye orodha hiyo. Awali kocha huyo alitakiwa kupewa kibarua cha muda wakati Mourinho alipofutwa kazi, lakini jina lake liliwekwa kando na Solskjaer akapewa kazi hiyo. Hata hivyo, Blanc yupo kwenye orodha ya wanawania kibarua cha kudumu cha kuinoa Man United.
Man United imeripotiwa pia kwenye majina hayo ya makocha wanaotaka kazi huko Old Trafford, yupo pia Julian Nagelsmann wa Hoffenheim.
Ni kocha kijana na hilo linaonyesha msimamo wa mabosi hao wa Man United katika kujenga timu ya kizazi kipya. Nagelsmann ni kocha wa kizazi kipya, mwenye mbinu za kisasa anayechuana na wakali kama Jurgen Klopp, Pochettino na wengineo akiwamo Pep Guardiola.
Jina la mwisho kabisa kwenye orodha hiyo ya makocha ndilo lililoshangaza wengi. Kuna kocha anaitwa Marco Rose. Kocha huyo wa Salzburg ameingia kwenye orodha hiyo baada ya kuifanya timu ndogo ya Austria kuwa tishio kwenye Europa League msimu uliopita, kocha huyo aliifikisha timu hiyo hatua ya nusu fainali. Alishinda pia ubingwa wa ligi na anaonekana kulirudia hilo msimu huu.
Rose alicheza chini ya makocha Klopp na Thomas Tuchel, hivyo ni kocha kijana kama Nagelsmann, ambao ndio watu wanaopewa nafasi kwa sasa kwa sababu akili bado zinafanya kazi kubwa.