Nooij aita 28 Stars kuelekea Kombe la COSAFA

Nooij aita 28 Stars kuelekea Kombe la COSAFA

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,229
Reaction score
610
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mart Nooij leo ametangaza kikosi cha wachezaji 28 watakaoingia kambini katika hoteli ya Tansoma iliyo eneo la Gerezani jijini Dar es salaam, kujiandaa na michuano ya kombe la COSAFA na kuwania kufuzu kwa AFCON na CHAN mwezi Juni mwaka huu.

Akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF amesema, wachezaji 28 aliowaita, amewaona kwa macho yake wakicheza, na katika wachezaji aliowaita amechanganya wanaochipukia (damu changa) na wenye uzoefu wa michuano ya kimataifa.

Nooij amesema katika orodha hiyo ya wachezaji 28 watakaoripoti kambini jumatatu mchana, watapimwa afya zao na madakatari wa timu ya Taifa, na kisha watakaokuwa fit atachagua wachezaji 20 watakaokwenda kwenye michuano ya COSAFA nchini Afrika kusini.

Aidha Nooij ameongeza wachezaji 8 watakaobakia nchini wanapaswa kuwa tayari wakati wowote wanaweza jumuishwa katika kikosi kutokana na Taifa Stars kukabiliwa na michuano mbalimbali ambayo pia inahitaji kuwa na wigo mpana wa wachezaji.

Wachezaji walioitwa na kocha Nooij ni magolikipa: Deogratius Munish (Yanga), Aishi Manula, Mwadini Ali (Azam), walinzi: Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Erasto Nyoni (Azam), Nadir Haroub, Oscar Joshua, Kelvin Yondani (Yanga), Abdi Banda, Hassan Isihaka (Simba), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Haji Mwinyi (KMKM).

Wengine ni viungo: Amri Kiemba, Salum Abubakar, Frank Domayo (Azam), Said Juma, Salum Telela, Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba), Haroun Chanongo (Stand United) na Mwinyi Kazimoto (Al Markhira).

Washambuliaji ni Ibrahim Ajib (Simba), Mrisho Ngasa, Saimon Msuva (Yanga), John Bocco, Kelvin Friday (Azam) na Juma Luizio (Zeco United).

Taifa Stars inatarajiwa kuondoka nchini siku ya jumatano, Mei 13 saa 1 jioni kwa shirika la ndege la Fastjet kuelekea nchini Afrika Kusini katika mji wa Rusterburg - North West Province ambapo ndipo michuano ya COSAFA CUP itafanyika kuanzia Mei 17 mpaka Mei 31 mwaka huu.

Mchezo wa kwanza wa Taifa Stars iliyopo katika kundi B katika michuano ya COSAFA, itacheza dhidi ya Swaziland Mei 18, Mei 20 (Madagascar Vs Tanzania) na Mei 22 ( Tanzania vs Lesotho), mshindi wa kundi B atacheza robo fainali dhidi ya timu ya Taifa kutoka Ghana.

Mara baada ya kumalizika kwa michuano hiyo, Taifa Stars itarejea nchini kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa AFCON 2017, dhidi ya Misri utakaopigwa Juni 13 nchini Misri, kisha kurejea nchini kucheza na Uganda Juni 21 kuwania kufuzu kwa fainali za wachezaji wa ndani CHAN.

Mart Nooj amesema ataitumia michuano ya COSAFA kama sehemu ya maandalizi ya michezo ya kuwania kufuzu kwa AFCON na CHAN.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Mei 7, 2015
 
So Msuva ataungana na timu S.africa............
 
Wtf hivi hawa akina Kiemba bado wanachaguliwa tuu what about dogo wengine wengi tuu ? Si bora hata kuchukua ngongoti mmoja kama Boko au Mwaikimba ambao angalau wanapata namba ktk timu .....Wale madogo viungo wa Mbeya City, Mgambo, nk hawaoni ? Huyu nae hamna kitu basi tu ..!!
 
Huyu kocha poyoyo sana, kiemba, bocco na mwadini wameitwa kwa kufuata mfumo gani!!
Jamaa wamechoka sana, halafu eti anawaacha akina mkude, Juma Abdul, busungu?!
 
Eti unamchukua kiemba na dida unamuacha bartez huu si wendawazmu!
 
Huyu kocha poyoyo sana, kiemba, bocco na mwadini wameitwa kwa kufuata mfumo gani!!
Jamaa wamechoka sana, halafu eti anawaacha akina mkude, Juma Abdul, busungu?!

Hakika nami nimeshangaa sana,tufike hatua tukatae eti unamchukua dida unamuacha barthez!!
 
Kila la kheri TAIFA STARS




Yaan ata iweje inabidi tuipe sapport timu yetu
 
daaaah hadi MKUDE KAACHWA tz ishaaga hayo mashindano
 
daaaah hadi MKUDE KAACHWA tz ishaaga hayo mashindano

Aiseeee Tanzania kila sekta pasua kichwa, yaani unamuacha Mkude panga pangua pale simba eti unakuja kuliita lizee hata halieleweki sijui linachaza bendi gani hapa bongo Kiemba!!!
Pale azam hapati nafasi halafu unamuita taifa!!!

Kocha la ajabu sana hili.
 
Yote 9, kumchukua KIEMBA sielewi sababu ni nini? mtu hapati namba, au ni kuwa timu zingine hazina wachezaji?
 
Back
Top Bottom