Sikirimimimasikini
JF-Expert Member
- Dec 27, 2019
- 2,926
- 15,634
North Korea imefanya jaribio la kurusha kombora la balistiki la masafa mafupi toka kwenye nyambizi (submarine) jana October 19, 2021.
Jaribio hilo limefanyika ktk kipindi ambacho wajumbe maalumu wa Marekani, South Korea na Japan ktk maswala ya North Korea wakijiandaa kukutana kujadili mpango wa silaha za nyuklia wa North Korea.
White House, Ikulu ya Marekani, imeiomba North Korea kusitisha majaribio yake hayo kwa kile (Marekani) ilichokiita vitendo vya kichokozi, huku msemaji wa Ikulu hiyo Jen Psaki akisema kuwa Marekani imeacha milango wazi ya kujadiliana na North Korea kidiplomasia juu ya kusitishwa kwa mpango wa silaha za nyuklia wa North Korea.
Chanzo: N.Korea confirms submarine launch of new ballistic missile