Not So Fast: Collabo ya Diamond na P-Square bado haijatoka

Mtamile

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2011
Posts
2,838
Reaction score
1,274
Kama umedownload au kutumiwa wimbo unaosemekana kuwa ni wa Diamond featuring P-Square na pamoja na kuusikiliza kwa mara kibao ukashindwa kusikia sauti ya Paul au Peter Okoye, basi sikio lako halikudanganyi – hakuna collabo hiyo.

Wimbo huo unaitwa ‘Marry Me' ni wa Iyanya ambao kipindi muimbaji huyo wa Nigeria amekuja kwenye Fiesta mwaka juzi, alimpa nafasi Diamond kuingiza kitu kwakuwa alisafiri na producer wake, Tekno aliyetembea na vifaa vya muhimu vya studio. Kwenye wimbo huo Diamond hakuimba serious na infact aliimba freestyle tu, kwa mujibu wa maelezo ambayo meneja wa Diamond ameyatoa kwa Bongo5.

Wimbo original upo kwenye album ya Iyanya iitwayo ‘Desire' (Iyanya vs. Desire) iliyotoka February 6, 2013. Kwahiyo Iyanya alitaka kutengeneza remix ya wimbo huo ambayo hata hivyo haikuweza kujumuishwa kwenye album hiyo.

Blog kadhaa za Bongo zimeupost wimbo huo kama wimbo wa Diamond aliowashirikisha P-Square kitu ambacho si kweli. Hakuna shaka kuwa hiyo ni collabo inayosubiriwa kwa hamu sana.


Source: Bongo5
 
Promo,kama kawaida yake kuvujisha nyimbo kupima upepo
 
domo ni kenge mumaji sana hakuna anayesubiria collabo yake na psquare.
 
Duh tuna safari ndefu sanaaaa kufika nchi ya ahadi kama tunajipa promo za kibwege kama hizi BTW sijausikia wimbo ila nilishatoa pongezi zangu nikijua ni kweli.
 
Duh tuna safari ndefu sanaaaa kufika nchi ya ahadi kama tunajipa promo za kibwege kama hizi BTW sijausikia wimbo ila nilishatoa pongezi zangu nikijua ni kweli.

Nadhani anataka kuwaandaa watu wawe na hamu zaidi ya kusikia wimbo wenyewe halisi kama atakuwa na mpango kweli wa kufanya collabo na P-Square
 
Ni mkali sana hata hvyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…