Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Tangu mwaka 2011, Novemba 17 imetambuliwa kama Siku ya Watoto wanaozaliwa Kabla ya Wakati Duniani ili kuongeza ufahamu na uelewa wa tatizo hili, pamoja na mahitaji na haki za watoto wachanga na familia zao.
Pia kuongeza uelewa wa umuhimu wa uzoefu na huduma za mfumo wa Afya na hivyo, kuendeleza sera zinazohakikisha haki na kupigania za #WatotoNjiti na familia zao.
=====
Mtoto aliyezaliwa hai kabla hajakamilisha wiki 37 za ujauzito huitwa mtoto njiti. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, watoto milioni 15 huzaliwa kila mwaka duniani wakiwa njiti, hii ni wastani wa mtoto mmoja katika kila watoto 10 wanaozaliwa.
Baadhi ya mambo yanayoweza kufanya mtoto azaliwe akiwa njiti ni -
Hakuna njia ya moja kwa moja anayoweza kuitumia mwanamke ili azuie kabisa kupata ujauzito utakaofanya ajifungue mtoto njiti, lakini mambo yafuatayo yanaweza kusaidia-
Baadhi ya dalili hizo ni kutokwa na damu kwenye via vya uzazi baada ya wiki 28 za ujauzito, maumivu makali ya tumbo yanayoashiria uchungu wa mapema wa uzazi, maumivu makali ya kiuno pamoja na kupasuka kwa chupa ya uzazi.
Chanzo: WHO/ Cleveland Clinic

- Magonjwa sugu kwa mama mfano Kisukari
- Uwepo wa maambukizi makali ya vimelea vya magonjwa
- Ujauzito wenye watoto zaidi ya mmoja
- Shinikizo kubwa la damu na kifafa cha mimba
- Uwepo wa changamoto kwenye kondo la uzazi na mlango wa kizazi
Hakuna njia ya moja kwa moja anayoweza kuitumia mwanamke ili azuie kabisa kupata ujauzito utakaofanya ajifungue mtoto njiti, lakini mambo yafuatayo yanaweza kusaidia-
- Kuepuka uvutaji wa sigara, madawa ya kulevya na pombe wakati wa ujauzito
- Kula mlo kamili
- Kufika kliniki za uzazi mara kwa mara
- Kusubiria walau miezi 18 tangu ujifungue kabla ya kupata ujauzito mwingine
- Kutunza uzito sahihi wa mwili pamoja na kudhibiti shinikizo la damu na kisukari