NOW AVAILABLE: "Majeruhi wa Mapenzi" - Pata Nakala yako sasa...

i will be the first one to buy 🙂
M.Mwanakijiji hongera sana mkuu.. Keep up great job..
Looking forward to read that book.

asante sana dear; nashukuru kwa kunitia moyo maana si kazi rahisi kama ambavyo nilidhania. Shukrani; usiwasahau wale rafiki zetu wa pande hizo!
 
Lol! Hardcore porn unanunua $ ngapi?

Good question! But coming to think of it, hard porn from M. M. Mwanakijiji......eewww, bure ghali!

Mtu yoyote anaefikiri anaweza kufanya kazi ya sanaa, kuitoa kwa umma, na kutokosolewa kwa njia moja au nyengine ni delusional
 
sasa unaweza vipi kukosoa kitu ambacho hujakiona; now that is delusional! Kwa sababu unakosoa kitu cha kufikirika! Umekaa ukafikiria ni porn; na hivyo ukakosoa porn! I mean if that is not delusional then what is?
 
Mkubwa sasa unakana kazi yako mwenyewe?! Sie wewe uliyetuwekea sura ya kumi na utambulisho wa sura ya kumi na moja?
 
Mkubwa sasa unakana kazi yako mwenyewe?! Sie wewe uliyetuwekea sura ya kumi na utambulisho wa sura ya kumi na moja?
Kitabu kina sura ishrin na tano kile, mkuu
Ungekisoma kwanza kabla ya kutoa critics
 
Kitabu kina sura ishrin na tano kile, mkuu
Ungekisoma kwanza kabla ya kutoa critics

Mwandishi anapoweka wazi sura moja wapo kati ya nyingi alizoandika, huwa anachagua ile aonayo inawakilisha vyema kazi yake.

Sisi tumeletewa sura ya kumi iliyojaa ngono laini, kwa hiyo kitabu hiki hata kiwe na sura saba wa sabiini, haijalishi, kitabebwa na sura ya kumi.
 
well, wewe kama hupendi ngono laini unapenda ngumu inabidi uzame huko huko kwenye ngumu ngumu...
 
well, wewe kama hupendi ngono laini unapenda ngumu inabidi uzame huko huko kwenye ngumu ngumu...

Anavyopendelea Gaijin si cha msingi. Cha msingi ni "jee, bei ya kitabu hiko inahalis' au la?" Nionavyo, bei hiyo haihalis' kwa sababu:-

1. Kwa kitabu cha ngono laini (tena paper back) hiyo bei ni kubwa mno ukilinganisha na vitabu vilivyopo sokoni.

2. Lugha iliyotumika ni fyongo. Kwa hiyo, si kama mtu atapata manufaa ya kujifunza Kiswahili. Nitatoa mfano mdogo

Tanabahi:
Review uliyotuweka isemayo "Shigongo sasa kapata mshindani aliye saizi yake" inadhihirisha kuwa kuna makubaliano kwa wasomaji kuwa ni kitabu cha ngono laini
 
Nimekupata vizuri sana; thanks.
 
Can u believe this; nimepatiwa invoice ya milioni 129 kuchapisha hiki kitabu!!!! VAT asilimia 18... nadhani China ni bora zaidi
Nimeona kuna watu humu wanaona hiyo $13 (about sh 20,000) ni kubwa! Ili kurudisha tu gharama hii utahitaji kuuza si chini ya nakala 6,400! Si kazi ndogo sana hii.
 
?????????????????????????
 
Hongera Mzee Mwanakijiji...kuandika riwaya si kazi ndogo. Kama vitabu hivyo vingeweza kupatakina pia kwenye bookshops za East Africa, ingekuwa na msaada mkubwa pia.
 
Last edited by a moderator:
Hongera Mzee Mwanakijiji...kuandika riwaya si kazi ndogo. Kama vitabu hivyo vingeweza kupatakina pia kwenye bookshops za East Africa, ingekuwa na msaada mkubwa pia.

vitakuja kupatikana nadhani wiki ijayo tu; sasa hivi hata watu wenye Kindle baadaye leo wataweza kukipata...
 
Nimeona kuna watu humu wanaona hiyo $13 (about sh 20,000) ni kubwa! Ili kurudisha tu gharama hii utahitaji kuuza si chini ya nakala 6,400! Si kazi ndogo sana hii.

Kwa nchi ambayo nusu ya watu wake wanaishi chini ya dola moja kwa siku, kusema dola 13 ni kidogo, ni kutujejea, kwa sababu hiyo ni nusu ya pesa ya mwezi [bila ya kuzingatia PPP]

Kwa watu wanaoishi nje, dola 13 kwa kitabu cha riwaya ni nyingi mno, kwa sababu kwenye soko vipo vya waandishi mashuhuri na mahiri zaidi kwa bei nafuu.

Mnunuzi haelewi habari za uchapishaji, kwa sababu anajiuliza mbona waandishi wengine wanauza kwa bei nafuu?
 
Nimeona kuna watu humu wanaona hiyo $13 (about sh 20,000) ni kubwa! Ili kurudisha tu gharama hii utahitaji kuuza si chini ya nakala 6,400! Si kazi ndogo sana hii.

hata gharama sidhani kama itarudi hasa kama nikiamua kuchapisha nyumbani; maana ukichapa vingi na watu wanasema hawana utamaduni wa kujisomea utaingia hasara ya bure tu; ukichapa vichache gharama ya kila kimoja ni kubwa mno kiasi kwamba u'll be fighting to break even..
 
Reactions: SMU

ni wazo zuri kweli; kwa mtu kama huyo hapaswi kununua kitabu asije kufa njaa. Na zaidi ni kuwa kwa mtu wa namna hiyo hata kufikiria kununua kitabu ni luxury ambayo hawezi kutakiwa kujaribu. Yule mwenye uwezo wa hizo dola 13 atanunua tu kama hana uwezo hapaswi kununua. Na kama unavyosema kama anaweza kununua kitabu kingine cha waandishi mashuhuri kwa bei ya chini anapaswa kufanya hivyo.

Kwa sababu nyumbani kitauzwa karibu ya Tsh 18,000 ambayo ni nyingi sana kwa watu wengi kwa hiyo sitarajii watu wengi wanunue kwa sababu wengi ni maskini.
 
Mnunuzi haelewi habari za uchapishaji, kwa sababu anajiuliza mbona waandishi wengine wanauza kwa bei nafuu?
Kusema ukweli sina uzoefu sana wa bei za vitabu vya namna hii kwa hapa kwetu, kwa hivyo sipo katika position ya kusema kama hao wengine wanauza chini ya sh 20,000 au la (kwa vitabu vilivyochapishwa kwa gharama kama hii aliyosema MM). Lakini najaribu tu kuangalia, kama gharama za kuchapisha ni za viwango hivyo, ni wazi bei za vitabu zitakuwa kubwa pia.

Btw, unawezaje kuona sh 20,000 ($ 13) gharama kubwa kwa msomaji mtanzania bila pia kuona Sh 129m ya kufanya uchapaji wa vitabu ni kubwa pia kwa mwandishi wa kitanzania?
 
Btw, unawezaje kuona sh 20,000 ($ 13) gharama kubwa kwa msomaji mtanzania bila pia kuona Sh 129m ya kufanya uchapaji wa vitabu ni kubwa pia kwa mwandishi wa kitanzania?

Bila ya shaka yoyote gharama za uchapishaji kama ni hizo ni kubwa lakini mimi siwezi kuzizingatia wakati wa ununuzi kwa sababu
1. Sina uhakika kama hizo ni gharama za chini zaidi ambazo muandishi angeweza kuingia au la. Sijui. Ninakwenda na maneno yake tu. Sijui project manager wake alikuwa mzuri kiasi gani kukata gharama. Sijui.

2. Nikiambiwa kinauzwa dolar 13 Amazon, wakati huko Amazon kuna vitabu kama hivyo kwa bei ya chini zaidi, ninapata wasi wasi kuwa gharama hizo ni za kujitakia
 
Reactions: SMU

Hakuna kati yetu mwenye mamlaka ya kuwakatia watu 'fatwa' ya kile wanachopaswa na/au wasichotakiwa kufanya.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…