DOKEZO NSSF inapanga kumpelekea Mahakamani Mkandarasi Mkuu wa Reli ya SGR, Yapi Merkezi

DOKEZO NSSF inapanga kumpelekea Mahakamani Mkandarasi Mkuu wa Reli ya SGR, Yapi Merkezi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mkandarasi Mkuu wa Reli ya Kisasa (SGR), Kampuni ya Yapi Merkezi anatarajiwa kufikishwa Mahakamani kwa kile kinachodaiwa kutowasilisha fedha za michango ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ya Wafanyakazi wa Ujenzi wa Reli ya SGR kwa muda wa zaidi ya Mwaka mmoja licha ya kuwa Wafanyakazi wamekuwa wakikatwa kwenye mishahara yao makato hayo kila mwezi.

Baada ya Wafanyakazi hao kulalamika muda mrefu ikiwemo wengine kudai wanaachishwa kazi bila kuwa na malipo hayo, wakatumia Chama cha Wafanyakazi wa Migodini na Kazi za Ujenzi (TAMICO) kuwasilisha barua ya malalamiko na kuhitaji maelezo kutoka NSSF kuhusu hicho kinachoendelea.

Barua ya majibu ya NSSF kwenda kwa Katibu wa Kanda wa TAMICO yenye Kumbukumbu Namba NSSF/ILA/1010397/62 iliyoaandikwa Septemba 6, 2024 ikijibu barua yako yenye Kumb Na. TAMICO/KANDA/2024/1245 ya Septemba 3, 2024, imeeleza kuwa Yapi amekuwa na malimbikizo ya michango kwa muda mrefu.

Barua hiyo imeeleza NSSF ina mpango wa kumfikisha Mwajiri huyo Mahakamani na kuwa mchakato upo katika hatua za mwisho za utekelezaji.

Soma Pia: Wafanyakazi wa SGR (Lot 1) wafanya mgomo, washinikiza Mkandarasi awalipe stahiki zao ikiwemo NSSF

Pamoja na hivyo imeelezwa kuwa Yapi amekuwa akitekeleza maelekezo ya kulipa malimbikizo ya michango ya NSSF inapotokea Mwajiriwa ameachishwa kazi au ameondoka kazini.

Soma Pia: Barua ya wazi kwa Rais Samia kutoka kwa Wafanyakazi Wazawa wa Ujenzi wa SGR chini ya Mkandarasi Yapi Merkezi (Lot 1)
 
Mtego no 1

Barua hiyo imeeleza NSSF ina mpango wa kumfikisha Mwajiri huyo Mahakamani na kuwa mchakato upo katika hatua za mwisho za utekelezaji
 
Mtego no.2
Pamoja na hivyo imeelezwa kuwa Yapi amekuwa akitekeleza maelekezo ya kulipa malimbikizo ya michango ya NSSF inapotokea Mwajiriwa ameachishwa kazi au ameondoka kazini.

Hakuna kesi hapa watachomoalea hapo.. WANALIPA.. HAWJAWAHI KUKAIDI KULIPA!
 
Back
Top Bottom