Nilisikiliza mjadala wa NSSF Kenya nikaona kikokotoo chao kina endana endana na vya Nchi za wenzetu...
Fikiria Mfanyakazi wa Kenya hukatwa 5% ya Mshahara na muajiri humchangia 5% kufanya jumla ya michango iwe 10% lakini akistaafu hupata wastani wa pension ya nusu ya Mshahara wake kila mwezi
Hapa kwetu mfanyakazi huchangia 10% na mwajiri 10% kufanya jumla ya 20% (mara mbili ya Kenya); tungetumia kikokotoo kama cha Nchi za wenzetu, wastaafu wangefaidika sana na michango yao pamoja na uwekezaji wa michango yao tofauti na sasa...