Mzalendo07
Member
- Feb 24, 2014
- 71
- 120
Mie kama mmoja wa wachangiaji niliyeona adha ya NSSF nimeona ni wajibu wangu kupaza sauti labda anaweza tokea Kiongozi anayejitambua na kuamua kulibeba hili na kuwasaidia Wananchi wa Sekta binafsi wanaochangia Mfuko wa NSSF.
Shida wanazokumbana nazo Wachangiaji ni zifuatazo:
1. Ukiomba fedha zako za kujikimu unavyokuwa umeacha kazi ama umefukuzwa ama mkataba umeisha, NSSF wanasema wanakupa 33% ya mshahara wako tena baada ya miezi miwili kupita. Hiki kiasi ni kidogo sana mtu kujikimu tena akiwa na familia, kwa nini wasitoe asilimi 30% ya fedha iliyokuwepo alafu ndio waanze kukupa 33% ya mshahara wako kwa kipindi ya miezi 18 angalau hiko kiasi kinaweza kukusaidia kufungua biashara yako ndogo.
2. Mtu ukiwa umefanya kazi kwenye makampuni zaidi ya moja ,kipindi unaomba fedha ya kujikimu ya kutokuwa kazini wao wanaanza kutaka kuthibitisha michango yako ya makampuni ya mwanzo ingali kwao fedha ya michango inasoma. Sasa ayo makampuni yakiwa yamefungwa na hayapo tena Nchini wanashindwa kukupa fedha kisa wameshindwa kuthibisha. Swali ni kwamba wanachotaka kuthibitisha ni nini? Na kama hiyo kampuni imefungwa wewe mchangiaji kwanini udhulumike.
3. Wanaweza poteza satifiketi na barua ya kusitishwa ama kuacha kazi lakini wanataka wewe ulete nyingine na wakati mwajiri hawezi toa tena
4. Wastaafu wanasumbuliwa bila kujali unapotoka.
5. KWA KIFUPI NI HIVI NSSF HAWASAIDII MTU WAKATI YUKO KWENYE MAITAJI NA FEDHA ZAKE LAKINI WAO NDIO WA KWANZA KUZISUMBUA KAMPUNI KWENYE KULIPA MICHANGO YA WAFANYAKAZI MPAKA WANAWAPIGA PENATI WAKICHELEWESHA .