NSSF ni janga kwa wafanyakazi

NSSF ni janga kwa wafanyakazi

Nyumisi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2010
Posts
13,499
Reaction score
19,292
Kuna jamaa yangu alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni ya vifaa vya ujenzi, akapunguzwa kazi kutokana na hali iliyopo ya kiuchumi iliyokolezwa na janga la korona.

Kwenda NSSF anaambiwa hawezi kupewa mafao yake yote, aendelee kutafuta kazi au apewe asilimia 30 ya mafao yake. Sasa cha kujiuliza, kwa nini NSSF wasiwape watu mafao yao ikiwa wameachishwa kazi na barua za kuachishwa kazi wanazo ili zikawasaidie kujipanga kivingine?

Hawaoni wanawasababishia ugumu wa maisha wakati hizo pesa ni michango yao na waajiri? Au ndo hizo pesa zinazokwenda kuwekezwa kwenye majengo ili watu wapige 10% yao.
 
Mimi niliwahi kusamehe mafao yangu kutokana na process kuwa ngumu wakati ninachokifuatilia ni kiduchu tu.
 
Serikali imechota hela imepeleka kwenye miradi mikubwa ba haijarudisha, Serikali hiyohiyo imewashurutisha Mashirika ya umma kuhamia kwenye nyumba zilizochwa na wawizara au taasisi zilizohamia Dodoma. haya magofu ya NSSSP, PSSSF nan anapangisha?
 
Muulize alimpigia kura Magufuli? kama akisema ndio mwambie anavuna alichopanda kwa hiyo atulie dawa iingie.
 
Serikali imechota hela imepeleka kwenye miradi mikubwa ba haijarudisha, Serikali hiyohiyo imewashurutisha Mashirika ya umma kuhamia kwenye nyumba zilizochwa na wawizara au taasisi zilizohamia Dodoma. haya magofu ya NSSSP, PSSSF nan anapangisha??
Miradi mikubwa serikali inatumia fedha za wachina na mabeberu.
 
Ela zetu za nssf zimekuwa kama ela za sadaka. Wanjichotea bila huruma.

Wanajengea magofu ambayo hawayatumii mwsho wa siku zinakuwa nyumba za mapopo kwa sbbu ela hzo hawajatolea jasho.

Pesa zetu zimekuwa za miradi ya papo kwa hapo.. Kiongoz akijickia tu anaenda kuchota ela.

Siku unastaafu au unaachishwa kazi unazungusha mpka bas. Pesa yako mwenyewe inakutesa.
 
Ni uonevu mkubwa sana. Wabunge wanapewa mafao yao yote tena mamilioni. Sisi wanaotuita wanyonge kupewa mafao ya milion 10 tu eti mpaka tuzeeke.
 
si mliwachagua wenyewe na wengine mlisaidia kuiba kura leo hii wacha msome namba
 
Ukiondoa wasanii na MaDC, Maelfu ya vijana- hawana ajira...Speaker na Mawaziri wanasema tu vijana mkajiajiri..But how? #UVCCM -kazi yao ni kupambana na Upinzani? hoja zao za kushawishi vijana ni zipi?

Sasa Wafanyakazi ni lazima waungane na vijana kudai #KATIBAMPYA

Baadhi ya Sera/Sheria mbovu za nchi ni kuwanyang’anya vijana uwezo.

Hapa naongelea vijana kuminywa kwa kuporwa haki zao, kunyimwa haki na kupuuzwa (hawasikilizwi). Naanza kwa Kuongezeka kwa Deni la Taifa na Propaganda mfu za Serikali, zenye lengo la kuhadaa umma ili kubaki madarakani tu. Serikali ya AWAMU YA 5 ilitamka kuwa inajenga miradi mikubwa kwa FEDHA za ndani. Asilimia kubwa ya Watanzania waliamini na kushangilia, na wale wachache wenye uelewa hawakupewa nafasi ya kuhoji. Imekuja kujulikana kuwa, FEDHA za Mifuko ya Jamii zilichukuliwa na Wafanyakazi wakaporwa haki zao za kulipwa #NSSF FAO LA KUJITOA na kuchelewesha malipo ya Wastaafu.

Vijana wasomi, waliosoma sayansi na wenye ujuzi wameajiriwa kwenye Makampuni, Mashirika na Viwanda. Hizi ni talent, na hazina za wasomi kwa nchi, na walivyoajiriwa kwenye haya Makampuni na Viwanda, wamepata fursa ya kuongeza utaalamu na uzoefu. Hii ndio Econonomic interelligency ambayo Serikali ilipaswa kutumia ili kunyanyua uchumi wa nnchi through Innovation. Ajira na mikataba za hawa vijana (wenye utaalamu na uzoefu-Innovation) zilivyokoma, Serikali iliwanyima Akiba zao (PESA za NSSF). Kumbuka Serikali ilifuta fao la kujitoa mwaka 2018 na kuweka Fao la kukosa ajira. Watu wote skilled labour (wataalamu hawa), hawapewi akiba yao, Haki imepotea. Hawa watu wangelipwa fedha zao, wangeweza kujiajiri kwa kufungua makampuni, kujenga viwanda vidogo. Badala yake hawa skilled labour wanaambiwa wasubiri miezi 18 na kama hawataajiriwa, wakae hadi 55 years wastaafu.

Serikali ilitumia pesa za mifuko ya jamii (Kukopa au kupora kienyeji) ili kujenga miradi. Hapo awali serikali imesema inajenga miradi kwa pesa za ndani (propaganda)..Lakini ukweli wenyewe ni kupora haki za wafanyakazi vijana na mafao wastaafu. Pia Serikali ilikopa sana Nje na kwenye mabenki, ndio maana deni la taifa limepaa sana.

Serikali inapaswa kuwapa wafanyakazi akiba zao ili waweze kutumia skill zao na uzoefu waliopata katika makampuni/viwanda ili kufungua biashara mpya. Hii ndio namna ya kutanua wigo wa Kodi (MWugulu NCHEMBA TRA). Mitaji itatoka wapi ya biashara mpya kwa wazawa kama mikopo benki sio rafiki? Suluhisho ni Serikali kurejesha FAO LA KUJITOA NSSF na kulipa wafayakazi akiba zao kwa Haki.

Serikali inatakiwa kuwezesha vijana, kutoa International passport kwa graduate wote, ili wapambane fursa za ajira kokote duniani. Baadae watakuwa diapora kubwa inayotuma pesa Tanzania, kama ilivyo Zimbabwe, Kenya na India walivyoenda wengi Canada na UK. Serikali kurejesha Fao la Kujitoa, Hasa kwa Sekta binafsi, kwa kuzingatia kuwa Sekta binafsi Security ya ajira ni delicate sana.
 
Umemaliza kila kitu mkuu.
 
Back
Top Bottom