ELNIN0
JF-Expert Member
- Nov 26, 2009
- 4,161
- 1,476
Wakuu,
Nimetoka NSSF kuchukua kadi mpya sasa hivi pia nikapata kucheki salio langu, yaani wakinipa hizo pesa leo nina uhakika wa kuwa na nyumba ya kisasa.
Ombi langu kwa mifuko hii wangebuni miradi ili watuwezeshe na sisi wanachama wao tunufaike kwa mfano ujenzi wa nyumba za kisasa na kutukopesha sisi wanachama wake kwa riba nafuu wakitumia masalio yetu kama dhamana ya mikopo.
Kama hawatoi mikopo hata mi naona hakuna haja ya mamilion yangu wakae nayo wakati mi nahangaika kukopa benki wa riba kubwa, na hii ndiyo inachangia watu wakibadili mwajiri wanazivuta pesa sababu hakuna faida unapata zikiwa huko.
Kama kuna mtu humu anafanya katika mifuko hii ya jamii atupe ufafanuzi zaidi hasa hili la kuwekeza kwenye nyumba na kuwakopesha wanachama wake.