NSSF rekebisheni daraja la Kigamboni

NSSF rekebisheni daraja la Kigamboni

Scaramanga

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2020
Posts
490
Reaction score
704
Pamoja na kuwa tuna kilio kwa serikali kutuondolea malipo ya kuvuka daraja la Kigamboni, niwapongeze NSSF kwa kujaribu kuweka urataribu wa kulipa malipo ya awali kabla ya huduma ya kuvuka na kuweka njia maalum gate namba 5 litumike.

Mwanzo utaratibu huu ulipoanza kiukweli ulileta tija kwa watumiaji kwani uvukaji ulikuwa mwepesi na wa haraka.Ila kwa sasa umekuwa kero mno kwani watumishi pale darajani wamekuwa wakiruhusu magari kutumia gate namba 5 ambao hawajalipa malipo kwa awali.

Imekuwa kero sana kwa wale ambao wamefanya malipo kwa awali kukaa foleni na kuondoa dhana nzima ya kufanya uharaka wa kuvuka. Hii inafanya hata kuona ni ujinga kulipa malipo kwa awali.

Niombe wahusika kama mfumo huu wa kulipa kwa awali na kuwa na njia maalum umeshindikana tujue na kama mtu analazimisha tumia njia hiyo akifika alipe fine ya 5000 kama usumbufu.

Shida pia watu wenu wanaendekeza ukiwauliza wanasema mageti mengine kuna magari yanapita , sasa nini maana ya kulipa kwa awali ni kufanya unapte unafuu wa kupita kwa haraka wacha hiyo njia ipitiwe na waliolipa kwa haraka ili watakaotaka tumia nao walipe kwa wakati.
 
MFANO LEO TAREHE 21/02/2015 nyerere BRIGE kero nyingine inakuja endapo ukivuka kutokea kigamboni kwenda kariakoo /Posta kupitia bandari road, kuna wakati maroli yanafunga foleni njia yote ile kuanzia uhasibu mpaka malawi cargo, maroli yana panga foleni kuelekea kitopeni yard, TICTS na ICD's,

ukivuka daraja huwezi enda popote, option inayobaki ni kugeuza urudi kinyume nyume umewasha hazard hadi sehem ya junction kupita chini uende uhasibu au urudi mpaka wanapokaa wao magetini ili ukajianze upya sasa ujinga mwingine ni wanataka ulipe ili tuu ukageuze, NSSF wekeni OPTION kama kuna dharula watu wageuke bila kulipa kama walisha lipa mwanzo, au toeni tangazo kuwa njia ina foleni mbele hii ni HUDUMA ili msichukue hela ya mtu halafu anaenda kunasa kwenye foleni masaa matatu, Hii iwe ni service sio kuchukua hela tuu
 
Back
Top Bottom