Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Siku ya jumamosi tarehe 7/12/13 kuliandaliwa mkutano au tafrija au hafla maalum ya kuwakutanisha watanzania waishio sehemu mbalimbali nchini Uingereza. Mkutano huo ulidaiwa kuyatarishwa na kampuni ya usafirishaji mizigo iendayo nchini Tanzaia iitwayo Swift Freights UK Ltd ambayo inadhaniwa inamilikwa na mtanzania aitwae Abdul Faraj.
Mkutano huo ulikuwa unatarajiwa kuwakutanisha wawakilishi wa shirika la hifadhi ya jamii la NSSF ambao walikuwa wanakuja kuuza ushauri kuhusu mpango maalum uitwao WESTADI ambao unawahusu watanzania waishio nje ya nchi.
Mpango huo unatoa fursa kwa kila mtanzania kuweza kuchangia kwenye mfuko huo dola za marekani karibu 300 kila mwaka fedha ambazo zingesaidia katika nyakati za maafa kama kifo ambapo mwili wa marehemu unaweza kusafirishwa hadi nyumbani kwa gharama za kutoka katika mfuko huo pamoja na msindikizaji.
Pia kila mwanachama wa kutoka nje akiwa nyumbani Tanzania anaweza kupata huduma ya matibabu bure pamoja na watu wa karibu wanne ambao wapo nyumbani nchini Tanzania ambao wangeweza kusaidiwa kupata huduma za matibabu ya bure endapo wangehitaji huduma hiyo.
Pia shughuli hiyo ingeambatana na sherehe za kuadhimisha miaka 52 ya uhuru, ambayo kilele chake ni Jumatatu, tarehe 9 December mwaka huu.
Kwa mujibu wa matangazo yaliyobandikwa katika tovuti za Ankal Issa Michuzi na ile ya dada yetu Jestina George, shughuli hiyo ingefanyiwa katika ukumbi maafuru wa shughuli wa La Royale Banquenting Suites uliopo White Hart Lane, Tottenham kuanzia saa 1 jioni hadi saa tisa asubuhi.
Ilidaiwa katika tangazo hilo kwamba kiingilio kingekuwa ni bure na kungekuwepo muziki ambao ungepigwa na mmoja wa ma DJ maarufu nchini UK bwana Chambi na pia kungekuwepo bendi ya wanamuziki ambao ni raia wa Congo ambao wana makazi yao sehemu hiyo ya kaskazini mwa jiji la London.
Jambo la kushangaza na la kutia aibu ni jinsi ubabaishaji uliojionyesha waziwazi kuhusu jambo zima na utaratibu mzima na namna jinsi sisi watanzania hasa tuishio nje tunavyoshindwa kuelimika katika masuala kama haya ya kufanya iwe hafla, sherehe au shughuli maalum.
Jambo la kwanza ni kutoonekana wa wawakilishi wa NFFS ambao ndio wageni maalum wa shughuli nzima kwamba ndio wangekuwa wasemaji wakuu na watoaji ushauri na ufafanuzi wa mpango mzima wa NSSF kwa sisi watanzania tuliotaka kupata maelezo.
Je kama wawakilishi wa NSSF walikuwepo London kwa shughuli hii, je waliishia wapi na waisonekane ukumbini na kama walikuwepo lakini wakaamua kuondoka je ni kwa sababu gani?
Je ni nani alipewa jukumu la kuandaa shughuli hii maalum na ni nani amelipia gharama zote za matayarisho ya shughuli hii? Pia je mheshimiwa balozi wetu bwana Kalaghe alifahamu juu ya ujio wa NSSF nchini UK na kwa kiwango gani ameshiriki kuhamasisha watanzania kuhudhuria shughuli hii kupitia tovuti ya ubalozi?
Nimemwingiza mheshimiwa balozi kwa kuzingatia kwamba shughuli hii iliambatana na kumbukumbu ya miaka 52 ya uhuru wa Tanzania hivyo kuipa uzito wa hali ya juu shughuli hii hivyo kungekuwepo na ugeni rasmi , ugeni wa NSSF WESTADI na wageni maalum kutoka, je kama anafahamu hii ni kwa kiwango (capacity) gani?
Nikija kwenye shughuli yenyewe haikuwa ya kufana sana kutokana na wageni hafifu ambao pia walichelewa sana kuingia kwenye shughuli yenyewe mpaka kuanzia mida ya saa tano usiku badala ya saa moja kamili ya usiku kama ilivyopangwa.
Jambo la muda linatusumbua sana watanzania wa UK ambao kulingana na maisha tunayoishi na wenyeji tumeona jinsi muda unavyopewa kipaumbele katika kila mazingira lakini kwa hili tumeshindwa sana. Ni shughuli, sherehe na tafrija nyingi sana watanzania wa UK wanachelewa tena hadi masaa manne kiasi cha kuwaambukiza hata wasanii wetu akina Diamond ambae alichelewa sana alipofanya onyesho lake la mwisho pale Kenning Town ambapo aliingia saa saba unusu za usiku.
Nikirudi kwa mtayarishaji bwana Faraji na wageni wake wa NSSF inasemwa kwamba wageni hawa hawakuwepo ukumbini na pengine hawakuhudhuria kabisa sherehe yenyewe. Sasa je ni sababu zipi zilizopelekea hali hii ukizingatia kwamba hakuna taarifa yoyote ya kuomba radhi na kufafanua kidogo hali yoyote iliyotkea hadi kusiwepo shughuli ya WESTADI na badala yake wananchi waendelee kununua vinywaji na nyama choma na kusakata rumba?
Nikiwa mmoja wa watanzania ambao tumeishi Ulaya kwa muda mrefu najisikia aibu sana pale sisi watanzania tunaposhindwa kuandaa hata kasherehe ka watu hamsini tu achilia mbali 100 kwani tunaonyesha waziwazi jinsi tulivyozoea maisha ya ujanjaujanja na ubabaishaji na kibaya zaidi pale tunapokuwa ni wasomi.
Kama mtanzania yoyote ambae yumo humu JF na alihudhuria shughuli hii maoni yenu yanakaribishwa kwa lengo la kujitambua tupo wapi na tunakwenda wapi.
Watanzania wenzetu wa USA je mpango wa WESTADI umewanufaisha vipi na vipi maandalizi yake yalifanywa na nani?, tafadhali tujadiliane bila jazba.