Yaani ajira za bongo hazina maana kabisa tena serikali ndo upuuzi mtupu,unaweza kuitwa kwenye interview kumbe watu walishapatikana yaani wanafanya kama formality,utakuta wakubwa wameshapitisha vimemo na watu wameshapata kazi.Mfano hai kuna jamaa nafanya naye kazi hapa wizara ya afya,huwezi amini hata cheti cha kidato cha nne hakuwa nacho,kaingia kwenye interview hata kujaribu kuongea kimombo hamna kitu,cha ajabu baada ya hapo ilipigwa simu toka juu ikiagiza huyu mheshimiwa lazima apate kazi,na mwisho wa siku alipata na analipwa mshahara mkubwa tu ambao hata hauendani na elimu ambayo nathubutu kusema hana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Jamani kwa kweli hili nalo ni tatizo ambalo ni ugonjwa katika nchi yetu. Upendeleo na ubaguzi ni mkubwa sana nchi hii. Mimi nafanya kwenye shirika moja la umma. Mambo yanayofanyika kwenye idara ya IT na idara zingine kwa ujumla, inasikitisha sana. Mpaka wakati mwingine tunajiuliza hivi kweli MUNGU anaona yote haya?. Boss ameletwa na na mwenye company. Yaani watu wanaajiriwa kutoka nje na the way interview zinavyofanyika yaani MUNGU ndio anajua. Wengine wanaletwa kwa mtindo wa kuchukuwa mtu kutoka nje bila interview.
HR wanaagizwa kumwita mtu ambaye wanamtaka among watu kibao ambao waliomba nfasi zilizowahi kutangazwa kama formality. Na hawakuwahi kuitwa hata mmoja kwa kutangazwa kwenye magazeti. Na wenyewe wanaamua nani wanamtaka na wanampigia simu maana wanafahamiana.
Kisha anafanyiwa interview na mtu mmoja boss kiasi sio Director/ Team ya interview kama mnavyofahamu, laa. Baada ya mtu huyo mmoja akiishafanyiwa interview anapelekwa jina lake kwenye BOARD ili apitishwe. . Kumbuka hajafanya na wezake? Ni yeye tu pekee.
Lakini kumbuka watu wa ndani wapo na wana degree za siku nyingi tu!.
Hawa wanofanyiwa interview za namna hii ni marafiki wa Boss na wanapokuja hata namba ya kazi hajapata anapangwa kwenda kwenye kozi fupi nje ya nchi. Na watu wandani wapo ambao wanafahamu system ya mahali husika. Wafanyakazi wa ndani wanajiuliza sasa sisi tumeonekana hatuna labda CERTIFICATIONS, na hatujui mambo fulani wanaotaka wakubwa. Sasa tunajiuliza kama wanajua kila kitu kwa nini wapelekwe tena kwenye kozi fupi? Maana wasiojua ndio wangepelekwa kwenye mafunzo hayo ya vitendo lwapone magonjwa yao, lakini wapi!
Yaani ukichunguza ni mtu ameahidiwa ULAJI na akitoka ULAYA au jirani Africa wanarudisha FADHILA kwa safari za mara kwa mara kwa wakubwa wanao waajiri. Yaani kuna MAONEVU MAKUBWA NCHI HII ambapo unapotafakari unawaza mpaka unaingia kwenye dhambi na cheo hutapewa ukisema sema. WANAPEWA VYEO NA SAFARI NA UTAGUNDUA BAADAYE KWAMBA NI MARAFIKI ZAO AU NDUGU WA WAKUBWA. WAKIISHA AJIRIWA WANSEMA WENYEWE MIMI NIMEAHIDIWA SAFARI ZA MARA KWA MARA
Ninatafakari hivi DHAMBI hii yakubagua watu na kupendelea watu na kuajiri kinyemela itakwisha lini kwenye WIZARA, MASHIRIKA YA UMMA?
MUNGU ingilia kati DHAMBI HII INANUKA.......