Ntakusaidia Kukuza Biashara Yako Kidigitali (Kwa Ombi Dogo Tu)

Ntakusaidia Kukuza Biashara Yako Kidigitali (Kwa Ombi Dogo Tu)

Joined
Apr 5, 2024
Posts
81
Reaction score
117
Habari wanajamvi,
Mi kijana wenu leo nimekuja kivingine. Mungu amekuwa mwema kwangu, na mwaka huu nna azimio la kubadili maisha ya watu kutumia ujuzi wa teknolojia nlo nayo.

Kwa sababu zilizo nje ya mada ya leo, nimelazimika kuanza upya (nilipoteza kila kitu 2024). Ila, mwamba hang'atuki vitani kisa amejeruhiwa vibaya.

Kwa sasa, nahitaji intaneti zaidi ya kitu kingine chochote, na kwa sababu hiyo, nina ofa maalum:

Ikiwa utaweza kulipia gharama yangu ya intaneti (TZS 150,000 kwa mwezi - bila kikomo), nitakufanyia kazi bila malipo ya ziada. Kazi zangu nazifanyia mtandaoni (freelance work).

Huduma Ninazotoa

Kutengeneza website kwa ajili ya bidhaa au kufanya mauzo. Hii itafaa duka la aina yoyote inayotangaza biashara..
Point of Sale (Mfumo wa kurekodi na kutathmini mauzo) – Ili kurahisisha biashara yako.
Mafunzo ya Kidigitali – Jifunze Excel, ChatGPT, na maarifa ya kompyuta.
✅ Copywriting/Grant Writing – Endapo una idea na unataka kuwavutia wahisani/wafadhili na unahisi unahitaji mtaalamu wa lugha, ntakusaidia. Au kama unahitaji kuandika nakala mbalimbali zinazohusu biashara yako, ntakupa sapoti ya lugha ya kutumia.
Huduma za kusimamia mitandao yako ya kijamii (Social Media Manager) – Mimi ni mwandishi (copywriter). Ntakusaidia kutunga, kuschedule, kuengage, na kukupa matokeo mtandaoni.
Mikakati Nafuu ya Masoko ya Kidigitali – Ikiwemo mfumo wa kutuma SMS/Email kwa wateja kwa ajili ya:
🔹 Kukumbushia malipo
🔹 Kuwashukuru baada ya manunuzi
🔹 Kuwajulisha kuhusu matukio yajayo

Nani Anaweza Kushiriki?

🔹 Mtu yeyote mwenye nia na atakayehitaji huduma tajwa hapo juu.
🔹 Watu wa kwanza 5 watakaokubali ofa hii watapata huduma zangu.
🔹 Leta changamoto yako ya biashara au teknolojia, nami nitakuletea suluhisho.
🔹 Tufanye kazi pamoja kwa angalau miezi 3 hadi 6 (au muda wowote utakaoona unafaa).

Pamoja tunaweza...💡 Niandikie kwenye WhatsApp: +255742308110.
 
Kila la kheri mkuu

Kama utaridhia mkuu mimi ninatamani kujifunza hayo unayoyafanya wewe.

Naomba. Muongozo
 
Back
Top Bottom