Ntobi: Tumetoka kumuona Boniface Jacob Segerea, ana Furaha amenyolewa kipara cha Wembe lakini Ndevu wamemuachia!

Hizo ndevu zenyewe ni huruma tu imepita hapo ila inatakiwa zinyolewe zote na kwa sababu mmesema humu hizo lazima zinyolewe zote. Sifa ya Gerezani ni kukutoa umaarufu tu na hauna cha kuwafanya.
Kama mwele na ndevu hazinuki why mtu anyolewe?
 
Polisi ya Tanzania ni ya hovyo sn
 
Oh asante kwa kunirekebisha kwenye hilo, so mtoa mada anasema wamemnyoa, how comes or ni kuongezewa chumvi?
Ndiyo maana mahabusu ana haki zote kama raia asiye na hatia ndiyo maana anakuwa kwenye nusu kizuizi tofauti na mfungwa ambaye anakuwa kwenye kizuizi kamili.
 
kwahiyo ameomba tumpampanie na kwamba hatma yake iko mikononi mwetu, right?

Ndio aachage ubabe na ukaidi sasa kwa polisi, ngoja tuone namna tunavyoweza. Aamini Mungu atatoka tu 🐒
 
Ni muhimu watu kuelewa kwamba mtu akiwa mikononi mwa polisi huitwa mtuhumiwa (suspect) , akifikishwa mahakamani anakuwa mshitakiwa (accused person) na akipatikana na hatia ndiyo ataitwa mfungwa/mhalifu (offender).

Kwahiyo mtu akiwa kwenye stage ya kwanza na ya pili kama nilivyotaja hapo juu anakuwa na haki zote kama za raia asiye na hatia lakini unakuta baadhi ya askari aidha kwa kukosa uelewa ama vinginevyo wanawachukulia kama wahalifu kitu ambacho sio sahihi na ni kinyume kabisa cha katiba na sheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…