Nuh Mziwanda aweka hadharani elimu yake

falcon mombasa

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2015
Posts
9,189
Reaction score
9,299


Huwa ni mara chache sana utasikia staa au mtu maarufu kajitokeza au kakubali kuweka wazi kuhusu sehemu aliyowahi kuharibu au kufeli kwenye maisha.

Kwenye muziki wa bongofleva tunae Nuh Mziwanda ambaye pia ni boyfriend wa msanii Shilole.

Nuhu ameongea ukweli wa moyoni kwenye exclusive interview na millardayo.com na kusema >>> ‘Kwenye maisha yangu ninachojutia ni nilivyofeli mtihani wangu wa form IV nilipata Zero kabisa na sikufanya mitihani kama mitatu, yote hiyo ilitokea sababu ya muziki'

‘Nilikua mtoto mwenye akili sana na Mama yangu alikua anategemea nitakuja kuwa mtu flani mwenye elimu yake kwenye familia yetu na sio Mwanamuziki, nyumbani kwetu tuko watano na mimi ndio wa mwisho na nilikua nina akili sana kuliko wote na kuanzia la kwanza mpaka la saba nilikua sishuki kwenye Wanafunzi kumi bora‘ – Nuh



Kwenye sentensi nyingine Nuh anamalizia >>> ‘Kupata Zero Form IV ni jambo ambalo linanifanya nijute sana mpaka sasa, ningekaza ningekua nafanya muziki huku nikisoma lakini nilivyojua maswala ya muziki tu nikaachana na Masomo, najutia…. nilikuja nikarudia tena mitihani na nikafeli, inaniuma sana… kama ninavyokosea kiingereza sio kwamba napenda, ni shule hamna'

Nuh amesema kuna uwezekano wa kurudi shule >>> ‘shule ni kitu muhimu haikataliwi, ni kitu poa unakuwa Mwanamuziki alafu una elimu yako… na muziki naudai sana ndio maana naukazania sababu ulinifanya nifeli shule.
 
Huyu kweli shule hamna na akili pia hana, nani kamwambia kukosea kiingereza ndo inareflect kiwango cha mtu cha elimu?
 
Arejee class... Tena atasoma vizuri tu. Elimu ya watu wazima.
 
Baba failure kapata zero form 4 mama alikuwa mama ntilie muuza ubwbwa.
 
Genius wa familia yuko hivi?

Gadem le mburulaz walianzaga hivi hivi..:wacko::wacko:
 
Kijana kajitetea kwa point hovyo kabisa, umemaliza form four alafu kidhungu not reachable? Alafu eti nilikuwa na akili sana kuliko ndugu zangu wote, kwa mantiki hiyo basi hao ndugu zake ndo vilaza haifai mfano.
 
Arejee class... Tena atasoma vizuri tu. Elimu ya watu wazima.

Hivi huyu Mziwanda ni muimbaji au ni bongo muvi? km ni mbongo fleva kaimba ngoma gani? na km ni mbongo muvi kacheza filamu ipi?
 
Akasome tu kuanzia QT kwa 1mwaka form 4 mwaka mwingine atapunguza ziro na kuanza ngazi ya cheti
 
kweli wamekutana pipa na mfuniko!' ............ shilole pia nae empty set.
 
Kuna yule Ras Simba anayefundisha kizungu kwa wiki 3.Akasome huko tujue ukweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…