Nukuu adhimu ya mwanafasihi

Nukuu adhimu ya mwanafasihi

Uncle Araali

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2014
Posts
950
Reaction score
1,262
WASEMAVYO WANAFASIHI:

"...Kusema haya na haya, duniani kuna vilima na mabonde; kuna kupanda na kushuka; kuna mashaka na raha. Yote hayo hayaendelei, likawa moja tu hilohilo kila siku.

Unapanda kilima kwa mashaka,taabu,kuchoka na jasho kukutoka. Lakini kilima kina mwisho wake; haiwi kuwa utakipanda tu moja kwa moja; mwisho wa kilima utateremka bonde kwa raha na wepesi, na hata ukimaliza bonde hilo, kaa ukijua kuwa mbele yako kuna kilima kingine kinakungoja. Hivi ndivyo dunia inavyokwenda; baada ya dhiki, faraji, na baada ya faraji, dhiki.

..." ( Mohamed S. Abdulla: DUNIANI KUNA WATU)
 
Back
Top Bottom