Nukuu za hapa na pale

Nukuu za hapa na pale

DMmasi

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2020
Posts
561
Reaction score
900
Hellow!! mwana Jamii

Unaambiwa hivi

Ukiwa ni mkamilifu mkumbushe yule aliyepotea njia naye awe mkamilifu. Tuhimizane kuyaishi mema na kuyakemea mabaya. Kama mvua na jua vinawapata wote walio wema na wabaya. Basi usimwache mkosefu apotee ikishuka adhabu niyetu sote.

Jitahidi kuepukana na shari, dhuluma, fitina, wizi, zinaa na dhambi nyingine zote. Hakikisha lile unalomtendea jirani yako likitendwa juu yako halito isononesha nafsi yako. Siyo sifa ya mwanadamu kuogopwa kama mnyama wakutisha, kama gonjwa lilokosa tiba wala kama pori lenye kiza kinene.

Naamu tuishi vyema na watu kwani maisha ni watu na watu ni sisi
 
Back
Top Bottom