Nukuu za Mobutu

Basi Nenda

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2017
Posts
20,774
Reaction score
47,866
mwandishi; pia hutaki mapadre wajihusishe na siasa ?
mobutu; ni swala lisilo kubalika,kama ma padre wakigusisha pua zao kwenye siasa za ubelgiji,ni sawa na ni vizuri lakini kwa hapa [zaire] haiwezekani,siasa na dini ni vitu ambavyo havichanganyikani ,hata yesu mwenyewe alikua anatenganisha vitu,vya mungu tumpe mungu na vya kaisari tumuachie kaisari


mobutu;kulikua na mapinduzi ya serikali yalipangwa kufanyika september 30,na njia pekee walipanga waniue, siku 5 au 6 msaidizi wangu akanitaarifu tukafuatilia mmoja mmoja watu 29 wanajeshi na raia wamekamatwa
mwandishi ; kati yao ni majenerali 12 kati ya 29 kama sikosei,ni kiwango kikubwa
mobutu ; kwahiyo ?
mwandishi ; inaelezea kuwa ni jambo kubwa lililokubalika na wengi,
mobutu ; huwezi sema hilo ni jambo kubwa lililokubalika na wengi wakati jeshi lina watu elfu 60

MATOKEO YAKE WATU 13 WALIOHUSIKA WALINYONGWA ,mobutu aliwaambia waandishi wa habari kuwa lazima mfano utolewe na matukio kama hayo yatatokomezwa bila huruma yoyote na hajali kuonekana katiri

MOBUTU KUHUSU DEMOKRASIA
mwandishi ; katika demokrasia yetu ya ulaya hatuui wala kuwanyonga wanasiasa
mobutu;rafiki yangu kipenzi ngoja nikukumbushe sisi sio wazungu sisi ni wabantu, usidhani kwa sababu mlitutawala basi tumekua wazungu na sisi,tunabaki kuwa wabantu na tuna nidhamu zetu ambazo sio zenu na kamwe hazitokua
mwandishi; kwahiyo demokrasia tunayoijua huku haipo ?
mobutu;tunaweza kuwa nayo ila sio saana, kwetu heshima kwa mtemi ni kitu cha lazima na kitakatifu huwezi mchezea mtemi,akiamua ameamua na inabaki hivo [mobutu alijiita mtemi] niliamua katika jina la jeshi kuwa tutakua madarakani kwa miaka mitano haikua wajibu wa wanasiasa kujiunga na wachumi kuleta machafuko ,walifanya hivo ikabidi tuwape mfano [kuwanyonga]


MOBUTU KUHUSU RUSHWA
mobutu ; hili sio janga lililopo zaire tu au limeletwa na wazaire ni janga linalopatikana nchini kote hata kwenu, nani katufundisha rushwa ? naamini ni nyie ,haikubuniwa zaire,ni bidhaa iliyoletwa kutoka nje [import] ndio maana tutapambana na huyu shetani kutoka nje

mobutu; mnasema mali za mobutu ni nyingi kuliko deni la nchi ,tunawachanganya watakao kuja kurithi mali zangu ,mali nyie wazungu mlizochuma zaire hakua mfalme leopold aliyezichukua na kuzitumia vibaya huku akituacha masikini ? wala hakua mobutu.kila nililoifanyia nchi yangu katika ujana wangu na nguvu zangu zote mnawaambia watu wangu nilifanya kwa ajili ya pesa ,niliyoyafanya sio kwa ajili ya pesa ni sababu ya uzarendo wangu


NB
mobutu alianzisha programme iliyoitwa salongo,kila week raia walitakiwa kufanya kazi mashambani kwa ajili ya taifa lakini wengi walikaidi,
mobutu alikua na sera yake ya haki,amani na kazi , alisisitiza raia wake wafanye kazi na kuna kipindi walifanya,zaire ikawa moja ya nchi tajiri zaidi yenye uchumi mzuri,lakini mwanzoni mwa miaka ya 90 alijitoa serikalini akaachana na shughuli za kuongoza serikali,akabaki kijijini kwake,serikali ikajenga miradi mikubwa ya umeme nk lakini wananchi mtaani walilia pesa hakuna huo ndio ukawa mwanzo wa kufa kwa zaire

wakati tanzania kukiwa na ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI ,pia zaire chama cha MPR WALISEMA ZIDUMU FIKRA NA MAWAZO YA MWENYEKITI WETU MOBUTU

kitu cha kujifunza kuhusu ZAIRE ni kuwa watu wanataka pesa mtaani sio miundombinu,
 
Kwa hiyo Unataka kusema Mobutu alikuwa mtu mwema?
 
mkuu, sijasema chochote, nimechukua tu historia kutoka documentary huko youtube
Kwa hiyo Unataka kusema Mobutu alikuwa mtu mwema?
ila nikujibu tu ni kuwa alipokuwa hai alisema, only history will judge me
 
Mkuu Unampenda Sana Mobutu ila alikuwa mtu mbaya sana
yeah mkuu, ni kweli marechal alikua na mabaya yake, mengine mi hua nayaona mazuri, mfano wewe hapo ulipo mtu akutongozee mkeo utamuacha salama ? mtu apange kukuua utamfanya nini ?, so ni kweli jamaa alikua na mabaya ila baadhi hakukosea kuyafanya, kuhusu utajiri mimi hua natamani kuwa nao kama wake then niishi kwa kutumbua sababu kuna wapuudhi wamewahi kuninyanyasa kisa sina pesa, nataka nije kuwa famous and successful kama mobutu ili nitafune papuchi kama alivofanya mobutu, mkuu inspiration comes from anywhere, ila shukuru mungu hujakutana na manyanyaso na mateso
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…