Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
NUKUU ZA NDUGU HUMPHREY POLEPOLE KATIBU WA HALMASHAURI KUU, ITIKADI NA UENEZI KATIKA MKUTANO WA HADHARA KATA YA MAKONGO JUU - KINONDONI
11 Oktoba 2020
1. "Nataka ndani ya hizi siku 7, mafundi wa Dawasco wawepo hapa kumaliza tatizo la maji, wasipofanya hivyo Chama Cha Mapinduzi tutalala nao ulalo ulalo". Ndg. Polepole.
2. "Tunapofanikiwa kama Nchi tutapata marafiki wengi na tutapata maadui wengi, Wananchi tuendelee kushikamana, kosa moja ambalo Rais Magufuli amefanya ni kusimamia ipasavyo maslahi ya Tanzania na kusimama imara tusichezewe na mtu yoyote".Ndg. Polepole.
3. "Wakati Rais Magufuli anaingia madarakani Tanzania ilikuwa inatambulika kama Nchi maskini, ndani ya miaka mitano hii tumeingia katika Nchi yenye Uchumi wa kati". Ndg. Polepole
4. "Hapa Tanzania kwa mara ya kwanza, Serikali kupitia Bunge ilifanya uamuzi wa kukopesha Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu fedha kupitia Halmashauri bila riba na uamuzi huu ulipingwa na wapinzani. Tunampongeza Rais Magufuli kwa kuwawezesha Wananchi wanyonge licha ya Wapinzani kupinga". Ndg. Polepole
5. "Tumenunua Ndege hawa watu wanasema tumenunua bajaji hivi ndege unaweza kufananisha na bajaji hawa watu wana nongwa tena nongwa za nywele ukikata zinaota tena". Ndg. Polepole
6. "Rais Magufuli ameanza kujenga Reli ya Kiwango cha kimataifa kutoka Dar es salaam hadi Dodoma ambapo ikikamilika itakuwa inatumia masaa 3 tu Dar hadi Dodoma, unaweza ukawa unaishi Dar unafanyakazi Dodoma". Ndg. Polepole
7. "Hapa Makongo mmechelewa sana mmechagua vimeo muda mrefu, Diwani na Mbunge ni wawakikishi na wahamasishaji wa maendeleo mnapokuwa na Diwani na Mbunge ambaye hataki kushirikiana na Serikali wanawachelewesha". Ndg. Polepole
8. "Nataka kuwatangazia kesho kutwa watu wa Barrick watakuja na pesa zetu zaidi ya Tshs. Bilion 100, wakati Ndugu Magufuli anapambana tupate haki yetu waliokuwa wanapinga ni hawa watu wa Chama cha Mbowe na Kabwe". Ndg. Polepole
9. "Amekuja Rais wa Malawi hapa anamueleza Rais Magufuli natamani nishike koti lako ukiwa unakimbia univute na mimi, hapo Kenya wanaomba Magufuli atawale hata Mwaka mmoja tu, maana yake wanamkubali sana". Ndg. Polepole
10. "Hao wapinzani maslahi wanayoyalinda ni ya mabeberu tu, Ilani ya Chama cha Mbowe inasema wataweka rehani madini yetu ili kupata fedha za miradi ya maendeleo". Ndg. Polepole
11."Hapa Jimbo la Kawe tunataka mtu mwenye mjumuiko wa hekima, busara, maarifa, uzoefu na nguvu nasi mwingine ni Bishop Gwajima". Ndg. Polepole
12. "Tumewaleteeni Mgombea Diwani kata ya Makongo Kijana kabisa ambaye anaweza akakimbia huku na kule kuhakikisha mnapata maendeleo, naombeni tumpe kura za ushindi Joseph Rwegasira". Ndg. Polepole
Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM.