Political Jurist
Senior Member
- Sep 6, 2021
- 143
- 120
NUKUU ZA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKIZINDUA KIWANDA CHA RADDY FIBER (FIBER OPTIC CABLE) MKURANGA PWANI.
"Urasimu katika uwekezaji ni suala ambalo halina nafasi kwenye serikali hii, nilishaweka wazi kuwa nchi yetu inahitaji wawekezaji kuliko sisi tunavyowahitaji, sisi tunawahitaji zaidi kuliko wao wanavyohitaji Tanzania".
"Mkongo wa mawasiliano wa Taifa ni mkongo wenye kasi kubwa unaowezesha mawasliano ya sauti picha na tarakimu au takwimu"
"Kuna Watanzania wengi ambao sasa wameshatembea wameshaona, wamepata mitaji, wamejikusanya wanataka kurudi nyumbani kuwekeza na kutuletea faida, naomba muwakumbatie kwa majina yoyote watakayokuja nayo akija Samia Suluhu we mpe awekeze"-
"Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya uwekezaji ikijumuisha, barabara, viwanja vya ndege, reli, nishati, umeme, gesi na maji, kwa sababu Pwani ni mkoa wa viwanda tunaenda kuupa umuhimu pekee kwenye masuala ya maji, nishati na gesi,"
"Tuko katika wiki ya vuguvugu la sherehe ya miaka 60 ya uhuru wetu, na katika wiki hii tumeamua kuchagua baadhi ya viwanda na miradi mikubwa ya kitaifa kuifungua au kuiwekea majiwe ya msingi na leo tumeanza na kiwanda hiki,"
"Serikali imeendelea kuweka Mazingira rafiki na wezeshi kuwezesha mawasiliano ya simu, mifumo ya Tehama na utoaji wa taarifa kwa umma kwa kuboresha, mawasiliano ya simu radio na runinga, ujenzi wa minara ya mawasiliano na kuendeleza ujenzi wa mkongo wa Taifa.
“Ndugu zangu , serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa ufanyaji wa biashara na uwekezaji. Tunafahamu bila mchango wa sekta binafsi hatuwezi kuleta mageuzi makubwa ya uchumi wa nchi yetu”
"Mwaka 2009 serikali ilianza ujenzi wa miondombinu ya ujenzi wa mkongo wa Taifa wa mawasiliono, sasa karibu tunakwenda kutimiza 75% ambayo tumeelekezwa kwenye Ilani ya Uchaguzi 2020/2025"
"Suala la usalama barabarani halina budi kupewa uzito mkubwa na kuwa ajenda ya kitaifa. Suala la ajali linamgusa kila mtu halichagui, naomba mlipe uzito mkubwa iwe ajenda ya taifa."
"Kwa kutumia Tehama serikali imweza kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo huduma za Kifedha (financial inclusion)".
"Kwa kiasi kikubwa Mtandao unasaidia sana kuleta urahisi katika kuleta maendeleo kwenye Taifa letu"
"Nmeambiwa kiwanda hiki kina uwezo wa kuzalisha na nmeona huko ndani, kiasi cha kilomita 24000 za waya zinazoenda kulazwa huko kwa mwaka na kinatazamiwa kuzalisha ajira 670 kitakapo kamilika kabisa".
#UwekezajiWaViwanda
#KaziInaendelea
[emoji1241][emoji1241]