Numbu je huu mmea unasafisha kweli figo na kibofu??? Sumu ya siafu na mmea(siujui jina) je ni tiba

Numbu je huu mmea unasafisha kweli figo na kibofu??? Sumu ya siafu na mmea(siujui jina) je ni tiba

Mhandisi Mzalendo

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2010
Posts
6,682
Reaction score
11,461
HABARI ZA SAA HIZI WANAJAMVI...
katika pita pita zangu huku mikoa ya nyanda za juu kusini nmekutana na dawa za jadi mbalimbali naomba kuuliza kama kweli ni tiba....

1. NUMBU
hii nimekutana nayo mbeya huku wakazi wa huku wanadai ni tiba mahususi kwa ajili ya kusafisha figo pamoja na kibofu na pia huongeza nguvu za kiume. Na pia mmea huu huwa wanautumia pale mgonjwa anapozidiwa humpatia na anapata nafuu.
JE WATAALAMU WA TIBA ASILI NI KWELI HUU MMEA UNATIBU HAYO???

2. SUMU YA SIAFU WENYE MABICHWA MAKUBWA
hii dawa nilikutana nayo wakati naelekea MPANDA . dawa hii huwa inatibu mifupa na kuondoa sumu aina mbalimbali kwenye mwili.
JINSI YA KUIPATA:
chukua siafu wajaze nusu kwenye glass ya maji ya kunywa halafu wawekee whisky kama vijiko viwili ile harufu ya whisky itawakera wale siafu na kuanza kutema sumu yao baada ya nusu saa watoe wale siafu na unywe ule mchanganyiko.
NOTE: muhimu ni ile sumu ya siafu na si ile whisky kwa hiyo kama una namna nyingine ya kuipata ile sumu itumie kuipata. Dawa hii ni maarufu sana china kwa maelezo niliyopata

WATAALAMU NAOMBA UDHIBITISHO KUHUSU HUU MCHANGANYIKO?

3. MMEA UNAOPENDWA NA VICHECHE
hii nilikutana nayo songea , vicheche na nyoka huwa ni maadui sana kwa hiyo mara kwa mara huwa wanapigana, kipindi wanapambana iwapo ikatokea nyoka kamuuma kicheche , kicheche huwa anakimbia na kwenda kuchimba mzizi wa mti flani, anaula ule mzizi na kurudi kupigana hapo anakua amepata kinga ya sumu kutoka kwa nyoka.
sasa huyu mzee niliyekutana naye akaniambia mzizi ule ni dawa nzuri sana kwa magonjwa mbalimbali na wazee wa zamani ilikua ndo dawa yao kuu.
JE MMEA HUO NI UPI NA HUWA UNATIBU NINI ??? NAOMBA KUJUZWA

NAWASILISHA KAMA KUNA MWENYE UFAHAMU NAOMBA ANIJUZE
 
Back
Top Bottom