Nunua bidhaa kutoka Mataifa 15 ikiwemo USA, UK, UAE na China sasa

Mwl.RCT

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2013
Posts
14,624
Reaction score
20,666
2024 | NUNUA BIDHAA TOKA MATAIFA MBALIMBALI DUNIANI NA MZIGO UTAKUFIKIA MAHALA ULIOPO

UTANGULIZI
  • Je, kuna bidhaa unataka kununua toka nje ya nchi kwa sababu hapa Tanzania umetafuta na hukupata?
  • Je, kuna huduma unahitaji kulipiwa mtandaoni?
  • Kama jibu ni NDIYO, basi hii thread inakuhusu.
Thread hii ni maalumu kwa wale wanaohitaji kununua bidhaa yoyote toka nje ya nchi. Bidhaa ambazo hazipatikani hapa nchini, au hata ukipata zinapatikana gharama yake huwa kubwa mara mbili zaidi, ukilinganisha na gharama ya kununua nje + gharama ya usafirishaji + kodi. Hivyo, thread hii itajikita katika nyanja kuu mbili:

[emoji778]1. BUY4ME : Manunuzi ya bidhaa mtandaoni toka mataifa zaidi ya 30:ikiwa ni pamoja na ITALY, UAE, CANADA, UK, USA, JAPAN, FRANCE, CHINA, INDIA, GERMAN, MALAYSIA, SINGAPORE, SPAIN & SOUTH AFRICA. Huduma hii nitaiita BUY4ME.

(a) Kupitia huduma hii ya Buy4me Utaweza kununua bidhaa kutoka katika masoko* yaliyo bora yasiyouza na kusafirisha bidhaa nje ya nchi zao.

(b) Pia ununuzi wa bidhaa toka masoko* ambayo yanaweza tuma bidhaa nje ya nchi zao, kuja huku Tanzania (Africa)

*Masoko = Online shopping site

Jukumu langu ni (i) KUKUNUNULIA (ii) KUKUSAFIRISHIA (iii) KUKUFIKISHIA mahala ulipo pindi bidhaa yako ifikapo hapa nchini.

[emoji778]2. PAY4ME : Malipo ya dharura ya hapo kwa hapo kulipia huduma na bidhaa.
Kutokana na kadi yako kuisha mda wake au kadi yako inashidwa kufanya miamala kwa wakati huo ambao unashida.
Yamkini upo safarini na unahitaji ufanyiwe malipo kwa haraka.
Na iwapo pia huna kabisa access na online payment system yeyote.
Huduma hii itajulikana kwa jina la PAY4ME .

Mfano:
Kulipiwa domain name, webhosting , licence keys kwa software au program yeyote uitakayo mtandaoni, kulipiwa huduma au uanachama katika tovuti mbalimbali mfano Netflix au HBO n.k

[emoji778] 3. SHIP4ME: - Ni huduma ya usafirishaji wa bidhaa toka mataifa 29 yafuatayo.
Amman
Barcelona
Beirut
Cairo
Cyprus
Dubai
FrankFurt
Geneve
Greece
Hong Kong
Instanbul
Jakarta
Johannesburg
London
Malaysia
Milan
Mumbai
NewYork
Ontario
Pakistan
Paris
Shangai
Singapore
South Korea
Sri lanka
Sydney
Tbilisi
Thailand
Tokyo
Je kuna mzigo wako upo katika hizi nchi ?, Au Kuna bidhaa unahitaji kununua mtandanoni kwenye hizi nchi? , Basi usisite kuwasiliana nami ili kufanikisha usafrishaji wa mzigo wako.


GHARAMA ZA SHIP4ME
  • Zinatokana na uzito wa mzigo (KG au LB ) bila kujali thamani ya huo mzigo.
  • Mzigo ukifika nchini iwapo utatakiwa kulipia kodi/ vat basi utajulishwa baada ya kupata mchanganuo toka mamlaka husika.

[emoji778]UTARATIBU WA KUNUNUA BIDHAA - BUY4ME

Utafuata hizi hatua

1. Tafuta bidhaa unayoihitaji toka tovuti tofauti tofauti.

2. Chagua bidhaa husika unayohitaji katika tovuti uliyo chagua mfano kama ni ALIEXPRESS, SOUQ, AMAZON (.com, .in, .uk ) au EBAY (.in, .com, .uk)

3. Nipe link ya hiyo bidhaa unayohitaji na uliyochagua.
Utanipa link kupitia email au whatsapp au PM

4. Nitaikagua link husika na Nitakujulisha gharama kwa TSH inayotakiwa kulipwa.

5. Utafanya malipo kwa utaratibu wa malipo uliowekwa.

6. Ndani ya dakika 5 - 45 tangu ufanye malipo nitakuwa nimelipia bidhaa yako na kukupa ushahidi wa:
  • Payment Invoice,
  • Picha (Screen shot) ya Bidhaa yako baada ya malipo kufanyika.
  • Uthibitisho wa email niliyopokea baada ya muamala kukamilika.
  • Hatua hii nitahitaji email yako au namba ya whatsapp ili kukutumia hivi vielelezo.

7. Utasubiri ndani ya saa 24 – 72 ili kupata tracking number ya mzigo wako kwa mizigo yenye tracking number.

8. Mzigo wako utachukua kati ya siku 9 – 21 kukufikia mahala ulipo.



[emoji778]GHARAMA UTAKAZONILIPA

- Kwa huduma ya BUY4ME utanilipa kwa makubalino baina yako wewe na mimi kutegemea thamani ya mzigo wako. Kiwango utakacholipa ni kati ya USD $5(Minimum) hadi USD $50 (maximum)

- Kwa huduma ya PAY4ME hii utalipia kiasi cha USD $5 hadi USD $25Tu.

- Viwango kwa TSH vitakokotolewa kulingana na EXCHANGE rate ya US dola kwa siku husika malipo yanafanyika.

- Ili kuona viwango vya kubadilisha fedhakwa manunuzi mtandaoni pitia hii link: Leo dola moja ni sawa na 2290. Kweli uchumi unakuwa - JamiiForums [ Update ya mara kwa mara itakuwa ikiwekwa hapo ]

[emoji778]MAKUNDI MAWILI YA TOVUTI MASOKO

[emoji778]KUNDI A
– Wauzaji wanatuma moja kwa moja bidhaa kuja Tanzania (East Africa) -
Ambapo gharama ya usafirishaji inajumuishwa wakati wa manunuzi ya bidhaa husika. (Napendekeza masoko ya kundi A yatumike Zaidi ili kupunguza ghalama.)

[emoji778]KUNDI B - Wauzaji wake hawatumi bidhaa kuja Africa, Nitawajibika kupokea mzigo wako katika nchi husika (viz UAE, USA, CHINA, JAPAN etl) .
Na mzigo ukishapokelewa ndipo unatumwa kuja Tanzania (Africa)
  1. Ambapo gharama ya kutuma Mzigo Tanzania (Africa) itatokana na uzito wa mzigo. Gharama HAZIKADIRIWI kwa mujibu wa mita za ujazo (Volumetric Weight W*L*H) (Angalia kipengele cha ghalama ya usafirishaji hapo chini)

  2. Tracking number utapewa mpya ambapo utaweza ku_track mzigo wako ukiwa Njiani kuja TZ (Africa).

  3. Waweza kutrack mzigo kwa njia Mbili (a) Kwa kutumia mfumo wa SMS katika simu yako, au (b) kwa kutumia tovuti kwa njia ya simu au computer.

[emoji778]GHARAMA ZA USAFIRISHAJI MZIGO – TOKA MASOKO KUNDI B

1. Iwapo umenunua bidhaa kutoka katika soko la kundi A. Gharama ya usafirishaji hulipwa wakati wa ununuzi.
Pia kwa baadhi ya masoko kwa bidhaa zote au baadhi ya bidhaa wauzaji, hutoa FREE SHIPPING, hivyo kunakuwa hakuna gharama ya ziada baada ya ununuzi wa bidhaa yako.

2. Iwapo umenunua bidhaa toka soko kundi B – Gharama ya kusafirishia hutegemea UZITO wa bidhaa husika katika KILO (Kg) au katika POUND (LB) na kiwango cha fedha hutokana na kila 0.5kg ya bidhaa yako. kwa huu utaratibu

[emoji778]Mfano:
a) 0.1 - 0.5kg Gharama ya kusafirisha ni USD 20.34
b) 0.6 – 1kg Gharama ya kusafirisha ni 33.14 USD
c) 1.1kg – 1.5kg Gharama ya kusafirisha ni 43.94 USD
d) 1.6kg – 2kg Gharama ya kusafirisha ni 56.74 USD

Hivyo pindi ununuapo bidhaa kwenye Soko kundi B – Hakikisha unaangalia uzito halisi wa bidhaa yako. Ili kujua kiasi cha fedha kitakacho hitajika kusafirishia mzigo.

Na gharama hii ya usafirishaji italipwa Pindi mzigo uondokapo kwenye nchi husika kuja nchini Tanzania.

[emoji778]NB:
1. Gharama ya usafirishaji yaweza kulipwa ndani ya SIKU 1 hadi 5 Tangu upewe taarifa ya gharama ya usafirishaji, kutoka nchi husika KUJA TANZANIA. ( Ni vyema ukalipa mapema).

2. Tracking number utakuwa nayo tayari hivyo utajua wazi mzigo wako umefika wapi au hatua ipi ya usafirishwaji.

[emoji778]KODI UTAKAYOLIPIA PINDI MZIGO UKIFIKA
  1. Pindi ununuapo bidhaa toka nje kumbuka kuna swala la kodi pindi bidhaa ifikapo nchini. (Kuna baadhi ya bidhaa huwa hazina nakodi – Mamlaka husika ndio huainisha bidhaa zipi zisizotozwa kodi)
  2. Utawajibika kwa malipo yote yatakayohitajika na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa bidhaa uliyonunua na iwapo utatakiwa kuilipia kodi.
  3. Gharama ya kodi hujulikana baada ya kuwa mzigo umekaguliwa na maafisa ushuru wa forodha hapa nchini.
  4. Iwapo kutakuwa na charges zingine Toka kwa shipping agent baada ya mzigo kufika utajulishwa na utawajibika kulipia.
  5. Malipo yote utakayofanya utapewa stakabadhi husika.
==
Kipengele #4

Iwapo kutakuwa na charges zingine Toka kwa shipping agent baada ya mzigo kufika utajulishwa na utawajibika kulipia.

Zingine Zipi hizo?
==
Angalia hiki kielelezo

- Iwapo mzigo umekuja kwa ndege, hizi charges #1, #3 na #4 zitahusika.
==
Na iwapo mzigo umekuja kwa njia ya maji ( Sea shipping ) basi huwa kuna charges zingine ambazo huongezeka na mchanganuo wake hutegemea na mzigo husika.
[emoji778]NJIA YA MALIPO (KUTUMA FEDHA)

Malipo yote yanapitia Benki, Chagua njia mojawapo kati ya hizi kufikisha fedha yako benki.

(a) Kwa kwenda benki na kuweka kiasi husika au

(b)
Kwa kutumia Mobile Banking - kwa mtandao wa Tigo au VodaCom (kama ilivyoelekezwa hapa chini)

[emoji778]MALIPO YOTE NI KWA NJIA YA MPESA / TIGO PESA KWA HUU UTARATIBU

1. Piga *150*00# AU *150*01# (kwa Tigo PESA)
2. Chagua 4. LIPA kwa M-Pesa na 4 kwa Tigo Pesa
3. Mpesa Chagua 4. Weka namba ya kampuni au Chagua 3 kwa Tigo Pesa
4. Tafadhali weka namba ya kampuni No. ( Utapewa )
5. Weka namba ya kumbukumbu ya malipo. (Nitakupa namba hii Baada ya kuwasiliana nami)
6. Weka kiasi (mfano: 50,000/=)
7. Weka namba ya siri.
8. Bonyeza 1 kuthibitisha:
** (BAADA YA MUAMALA KUKAMILIKA, TUMA KWANGU UJUMBE UTAKAOPOKEA- KAMA UTHIBITISHO)

[emoji778]NJIA ZA MAWASILIANO

Wasiliana nami kwa moja ya hizi njia
1. Kupiga simu/ Kutuma ujumbe: 0717 54 57 62 au 0788 203 160
2. Whatsapp: +255 788 203 160
3. Telegram: @MwlRCT

[emoji778]MUDA WA KUWASILIANA NAMI
1. 06:00 – 19:30hr (Saa 12:00 asubuhi HADI Saa 1:30 Usiku)– Simu/sms/whatsapp/telegram - Utajibiwa
2. 19:30 – 06:00hr (Saa 1:30 usiku HADI Saa 12:00 asubuhi)– Niachie ujumbe wa simu (sms)/whatsapp/telegram/email, Na utajibiwa au kupigiwa simu kabla ya 08:00hr Kila siku.

Iwapo unamazungumzo marefu na unahitaji kupigiwa simu niandikie kwenye ujumbe “CALL PAY4ME” au “CALL BUY4ME” na nitakupigia bila gharama yeyote.

IWAPO UNAWEKA LINK KWENYE HII THREAD TUMIA HUU UTARATIBU


Mfano jinsi ya kupata link ya bidhaa husika: BONYEZA HAYA MAANDISHI

[emoji815]BAADHI YA MAONI YA WADAU WA JF[emoji815]
Nashukuru sana ticha nlikua muoga snaa (3milin)kufany busnes na ww atimaye mzigo nimeupata ukiwa safiiii kabsa alichonifraisha zaidi uyu jamaa anajibu text kwa wakat whtsp and kila kitu kipo open
Nashukru sana Mwl kwani mzigo wangu wangu umefika salama.Mwanzoni nilikuwa na wasiwasi kama kweli ingewezekana hasa ukizingatia kufanya biashara na mtu usiyemjua.Ongera sana kwa huduma na uaminifu na bila shaka tutafanya biashara zaidi.
 
BAADHI YA TOVUTI ZITAKAZOTUMIKA KUNUNUA BIDHAA

Ziko tovuti nyingi, siwezi orodhesha zote, baadhi ninazopendekeza ni kama AMAZON & EBAY ( Bila kujali .com, .in au .uk )

CHINA



Masoko mengine kwa china ni kama ALIEXPRESS, ALIBABA n.k

JE NITAUPATA VIPI MZIGO WANGU BAADA YA KUWA UMEFIKA TANZANIA?

- Utapigiwa simu kukujulishwa kuwa mzigo wako umefika.

- Utaletewa ofisi kwa wale wanaoishi katikati ya jiji ya Dar es salaam, FREE DELIVERY. au

- Utaelekezwa mahala unatakiwa ufike ili uchukua mzigo - Ni city centre kwa walio Dar es salaam, Waweza kuja wewe mwenye au ukamtuma mtu akuchukulie.

- Kwa walio mikoani au nje ya Tanzania utatumiwa kwa njia ya EMS au kwa njia ya basi kwa kadri wewe utakavyo pendekeza njia ipi itumike – Utalipia hii ghalama.

Mifano hai:

1. Mteja Toka nje ya TZ (anaishi DRC) – Bidhaa yake imetoka China, Na alitumia kwa basi kwenda DRC.


2. Mteja ndani ya TZ anaishi Mkoani – Bidhaa yake imetoka UK

Wateja wote nimekutana nao hapa JF na hakuna tuliye onana ana kwa ana, Zaidi ya njia za mawasiliano tajwa hapo juu.

CHANGAMOTO

ANGALIZO
1. Usifanye malipo yeyote bila kuwasiliana nami kwanza, Kwa njia mojawapo ya mawasiliano tajwa hapo juu.

2. Haito tokea kupigiwa simu, au kuandikiwa ujumbe mfupi, kuwa fanya malipo kwenda namba Fulani ya simu.

3. Hakuna malipo yeyote yatakayofanyika kwa fedha taslimu kwa kukabidhiana mkononi.

4. Malipo yote ya fedha yatafanyika kwa utaratibu uliowekwa hapo juu.

5. Miongoni mwetu kuna wenye uoga na mawazo ya kuibiwa/ kutapeliwa pindi lijapo swala la fedha na swala zima la manunuzi mtandaoni.

Yaani kutuma fedha kwa mtu usie mfahumu/ kumuona/ asiye na ofisi mahala ulipo.
Na hujibainisha kwa haya maswali Ofisi yako iko wapi? , Uko wapi nataka nikukabidhi fedha mkononi au nataka tuandikishiane!

- ONDOA shaka, kwa kufuata taratibu zilizo ainishwa hapo juu, uko salama, Na bidhaa yako AU huduma utakayolipia utaipata.

- Iwapo UNA SWALI, PENDEKEZO au USHAURI wasiliana namI au andika kwenye hii thread.

KARIBU
 
Hongera sana Mwl.RCT kwa miaka karibu 6 nimekuwa mteja wa Huduma zako japo hatufahamiani kwa sura.

Kuna wakati nilifanya transaction ya mkwanja mkubwa hadi wife akaniuliza Kama Nina kichaa kutma kiasi hicho cha pesa kwa mtu usiyemfahamu.

Kweli uaminifu ni mtaji, naamini utafika mbali Sana!
 
Mkuu naitaj manual tread mill inaweza nigharimu shiling ngapi?
Gharama hutegemea ni:-

- 1. Brand ipi umechagua
- 2. Je ina feature zipi za ziada? mfano: Calorie Monitor etl
- 3. Njia ya usafirishaji itakayotumiaka.

Hivyo fungua EBAY au ALIEXPRESS
Code:
 www.ebay.com  au www.aliexpress.com
Kisha chagua model utakayoipenda.
Na nipe link yake, ili nikupe mchanganuo wa gharama kikamilifu.

Karibu
 
Mkuu toka nilivyoanza kuona post zako nmekuamin kwa asilimia kubwa zaid ya 74%

Ila ushauri tu, fungua office sehem kama huna, weka na kainternet cafe itakuwa njema zaid mkuu, na urahisi pia.. Yangu ni hayo tu teacher.
 
Mkuu toka nilivyoanza kuona post zako nmekuamin kwa asilimia kubwa zaid ya 74%

Ila ushauri tu, fungua office sehem kama huna, weka na kainternet cafe itakuwa njema zaid mkuu, na urahisi pia.. Yangu ni hayo tu teacher.
mwalim unatoa huduma nzuri sana ila bila ya kuwa na ofisi sehem.. unapunguza idadi ya wateja.. jitahid uww na ofisi
Shukrani kwa ushauri.
Karibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…