Naomba kufahamishwa wadau,kuwa unaweza kununua bidhaa nje ya nchi (online)mfano: nchi kama,UK,S. Afrika ,japan, china n.k kwa ajili ya matumizi yako na ukatumiwa kama parcel kwa njia ya Western Union au DHL bila kulipia kodi?? Mfano; Laptop,simu,camera,novel na bidhaa ndogo ndogo; naomba kufahamishwa wadau!!
Mi sijawahi kusikia western union wakisafirisha mizigo, leo ndo nasikia kwako. Bidhaa yoyote inayostahili kulipiwa ushuru utalipa bila kujali umenunua nchi gani au umesafirisha kwa shirika gani maana customs officers wapo kila mlango wa kutokea na kuingilia nchini.
Ila kuna baadhi ya vifaa kama hiyo laptop uliyotaja hailipiwi import duty (25%) ila inalipiwa vat tu (18%).
nashukru mkuu kwa kunikosoa,nilidhani western union nao wanasafisha Parcel.... kwa hiyo km novel na laptop pia zinalipiwa VAT na kwamfano hao DHL wanaweza kuniletea mpaka nilipo??na hiyo import duty inalipwaje na nani kwa hiyo parcel??
nashukuru pia kwa hilo mkuu...nimezi kuelewa zaidi.
naongezea hapo DHL wata kupigia simu kukujulisha kuwa kuna mzigo wako na unatakiwa kulipia kiasi fulani cha kodi so wewe uta ruhusu walipe then we we utawarudishia