Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
NURU BINT SUDI KUTOKA ''MAUTP WANA MAJAMBO TANU WANAICHUKIA'' (1957) HADI ''MAZAO BORA SHAMBANI'' (1967)
Nuru bint Sudi katika wakati wake alikuwa mwimbaji nguli wa taarab kwanza na Al Watan kisha akahamia Egyptian.
Hii ilikuwa miaka ya 1950 wakati harakati za TANU zimepamba moto wakipigiania uhuru wa Tanganyika.
Nuru bint Sudi alipohama Al Watan kwenda Egyptian mji wa Dar es Salaam ulitikisika kwani vikundi hivi viwili vilikuwa na upinzani mkali sana mathalan ya ushidani uliokuwapo kati ya Sunderland na Yanga.
Siku ya kwanza Nuru bint Sudi kuimba na Egyptian ilikuwa katika ufunguzi wa tawi jipya la TANU Mtaa wa Mvita.
Tawi hii lilianzishwa mwaka wa 1954 Kisutu na kufika 1957 wakaona itakuwa bora tawi lihamie Kariakoo bila shaka kwa kuwa Kariakoo kulikuwa na wanachama wengi wa TANU kupita Kisutu.
Siku ya ufunguzi viongozi wa tawi hili la Kisutu lililokuwa limehamia Mtaa wa Mvita, akina Haidar Mwinyimvua waliona itapendeza kama Egyptian itatumbuiza katika hafla ile.
Ikasadifu kuwa Nuru bint Sudi ndiyo kahamia Egyptian na ataimba katika hafla ile kwa mara ya kwanza na kundi lake jipya.
Naam.
Mtaa wa Mvita usiku ule ulifurika kote hadi Mtaa wa Livingstone na Msimbazi yake.
Nuru bint Sudi siku na usiku ule alimba nyimbo yake mpya, ''MaUTP wana Majambo TANU wanaichukia.''
UTP yaani United Tanganyika Party kilikuwa chama kilichoundwa na Wazungu kupambana na TANU na kwa ajili hii kikawa kinachukiwa na kila mtu aliyetaka uhuru wa Tanganyika upatikane chini ya TANU chama cha wazalendo kilichokuwa kikiongozwa na Julius Kambarage Nyerere.
Nyimbo hizi mbili za Nuru bint Sudi zimepishana kwa miaka 10.
Nyimbo ya ''MaUTP'' kwa hakika Egptian wasingeweza kuirekodi Tanganyika Broadcasting Corporation (TBC) kwa sababu zilizo wazi kabisa.
Kwa ajili hii naamini haipo kwa sasa.
Manju Masoud Masoud kaniletea nyimbo hii moja ya Nuru bint Sudi aliyoimba mwaka wa 1967, miaka 65 iliyopita nimsikilize nyimbo iliyorekodiwa ndani ta studio za RTD, studio yetu wenyewe baada ya Tanganyika kuwa huru mwaka wa 1961.
Uhuru ambao ulipiganiwa na wazalendo kama Bi. Nuru bint Sudi akitumia kipaji chake cha uimbaji.