SoC02 Nuru gizani

Stories of Change - 2022 Competition

Newrise

New Member
Joined
Jul 30, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Ndani ya giza nene lisiloweza kuruhusu aina yoyote ya mwanga kupenya ndipo vijana wenye uthubutu wakafanya kila bidii katika kuonyesha kile kilicho ndani ya fahamu zao ili kurudisha uaminifu tena. Ni miaka mingi imepita tulipokuwa tukishuhudia mafanikio ya wengi kupatikana katika siku zao za uzeeni lakini sasa imekuwa tofauti na zama hizo baada ya vijana kuamka na kuonesha jitihada katika kutafuta na katika uthubutu na kujihusisha na vitu vingi hasa vinavyohusiana na talanta walizonazo.

Vijana wengi wamekuwa wakikumbana na maneno mengi hasa kuanzia katika ngazi ya familia hadi jamii kwa ujumla maana wengi walikua wanaonekana si wasikivu na wanaenda kupotea lakini haikuwafanya wao kukata tamaa maana walijua na njia ipi iliyosahihi kwa ajili ha kutimiza malengo yao na hata wakafanikiwa kufika walipotaraji kufika na kuwa wahamasishaji mashuhuri kwa vijana wenzao pia.

Vipaji ni vitu muhimu sana katika kumbadilisha mtu toka hali moja hadi nyingine kama zilivyo nyenzo zingine kama elimu, lakini nyenzo hii ya vipaji imekua ikikosa misingi madhubuti katika Taifa letu na kufanya ndoto za wengi kufa hata kupoteza muda mwingi katika vitu wasivyoviweza.Wengi wamekua wakidharauliwa hata katika jamii zao endapo wameamua kuacha elimu na kujikita katika kuimarisha vipaji vyao vya ndani ambavyo vimekua na fyrsa nzuri sana katika nchi zilizoendelea hata kuinua uchumi wa nchi hizo ikiwemo Marekani na nchi nyingi za ulaya.

Taifa letu na uongozi wote kwa ujumla lingeangalia sera nzuri katika kuhakikisha linalea vipaji vya watoto wengi ndani ya taifa letu hata kutoa fursa katika kuwakilisha ubunifu walionao katika mashindano mbalimbali kama vile mashindano ya kuchora,kuchonga vinyago na mambo mbalimbali.

Tukiangalia muziki kwa sasa umeweza kulitambulisha taifa sehemu mbalimbali kupitia wasanii waliopambana katika kuonyesha ustadi ndani ya kazi zao kama vile Diamond Platnumz,vipaji vikiwa sehemu ya kipaombele cha taifa katika kuwainua vijana itasaidia kupunguza msongomano wa watu wengi katika vitu wasivyoweza na mtu kutambua sehemu anayoimudu ili iweze kumpa faraja kwa siku zijazo na kuendesha familia yake.

Pia kitakua kitu cha kupewa heshima kwa watu wengi ivyo kuwapa kujiamini vijana wenye kujikita ndani ya fursa za vipaji vyao maana wengine wamekua wakiogopa kuingia katika mziki wakiamini ni uhuni la hasha si kweli,hivyo kukiwa na usimamizi madhubuti vitakua ni vya vitu vya heshima katika jamii kwa ujumla.

Ongezeko la fursa katika nchi ni chanzo cha kupunguza idadi ya matukio hasi yanayotokea katika jamii kama wizi na matendo hatarishi maana wengi watakua wamejikita katika utafutaji na kujiweka katika nafasi ya kupata vipato vizuri,pia zikawepo shule zenye kusimamia vipaji hivyo kama shule za soka zinazotambulika kiserikali zitaongeza chachu hata uaminifu kwa wazazi kuwaruhusu watoto zao katika kujiunga na kuwafanya waziishi ndoto zao.

Tumekuwa katika mazingira ya kuamini shule tu inatosha lakini vipi kwa wale wasioweza mashuleni na wanweza katika vipaji vyao ni wakati muafaka wa kupanua mipaka ya kifikra na kuwawezesha watu kufika katika hatima zao chanya walizozikusudia.Kwa wakati tulionao shuhuda ni nyingi kupitia wale waliofanikiwa katika hili hatuna la kupoteza kwa maana muda sahihi ni sasa na wakati sahihi ni huu katika kulitimiza hili ili kuleta mafanikio kupitia vijana wenye vigezo na wenye sifa katika kulitimiza hili na kuondoa mitazamo hasi kuamini mafanikio yapo katika njia moja hasa elimu. Vijana wengi wamekuwa wakifa na ndoto zao kwa kusosa misingi mizuri, kwa kukosa washauri, kukiwa na misingi mizuri kiuongozi vijana watajua wapi pa kuanzia katika kuomba nafasi kwa ajili ya kuendeleza vipaji vyao.

Jambo hili la vijana kutumia vipaji vyao likiwekea sera na kuhamasishwa na watu wakubwa kama rais itasaidia kuongeza shauku ndani ya vijana na kutumia vizuri vile vilivyo ndani yao katika kuelimisha, kuburudisha na kuongeza mshikamano katika jamii,hata kuliwakilisha taifa kiujumla na kuongeza pato la nchi.Pia Serikali kuendeleza mipango madhubuti kama kutoa elimu kwa vijana jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii vizuri katika kutangaza kazi zao na jinsi ya kuvuna matunda ya kazi zao itasaidia vijana wengi kufikisha kazi zao ulimwenguni kote kiurahisi kulingana na karne tuliyopo ambayo mambo mengi yanaenda na utandawazi, hivyo elimu juu ya faida ya utandawazi itasaidia kuwaweka katika daraja zuri la kuyafikia mafanikio wanayoyatamani kwa muda mrefu.
 
Upvote 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…