Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Binadamu na utukufu wake wote au uovu wake wote, mwisho wake ni kifo. Wote tutazikwa kule, Maskini kwa tajiri kifo hakichagui. Kinatenda haki kwa wote.
Muda wetu wa kuishi duniani ni mfupi mno na unakimbia balaa. Nyakati za utoto na ujana zinapita kama mshumaa na tunajua wote ni lazima tuwe wazee.
Na uzee unapokuja ndio unajua kifo kinakaribia. Nguvu zako zitakapoanza kupotea na kumbukumbu kutoka.
Kama maua waridi unayaona leo mazuri kesho yananyauka ni kama ujana tu.
Urembo wa kijana wa kike au utanashati wa kijana wa kiume hawezi kukaa nao milele, tunabadilika kotoka utoto, ujana na uzee.
Uzuri hauwezi kukaa ndani yetu milele, wala nguvu tulizokuwa nazo wakati vijana hazitodumu.
Kama majani yanavyochipua na kunyauka kisha majani mengine kuota ndivyo kizazi hiki kitavyopotea na kizazi kingine kitachipukia.
Tumeona watu wengine ambao tulikuwa nao, walikuwa miongoni mwetu, hatunao tena. Wameishafariki. Hawapo hatuwaoni. Yamebaki mabaki makaburini.
Kwetu sisi ambao tumebaki tunaendelea kupumua ni lazima tujue kitu kimoja. Kama jua linaendelea kutuwakia kila siku na unavuta hewa na kutembea juu ya ardhi hii. Hauna budi kushukuru. Na kuacha kujisahau.
Mvua inaponyeshea ardhi ; Majani hukua na mazao tuliyopanda hushamiri. Majani kwa mifugo ambayo tunafuga kwaajili ya maziwa na kitoweo. Na nafaka kwaajili ya chakula chetu cha kila siku ili tuendelee kuishi. Sisi binadamu hatuwezi kuendelea kuishi pasipo chakula.
Kitu kimoja lazima tujue ni muhimu kumheshimu Mungu anayetupa vyote hivi na aliyetuweka kwenye ardhi hii tuishi. Kitu cha muhimu ni kuishi kwa busara. Ili tufanye dunia hii ambayo tumepewa kuwa mahali salama pa kuishi.
Ni Muhimu sana kumheshimu Mungu na kuheshimu binadamu wenzako. Mbali ya rangi zetu na kabila zetu tunachangia kitu kimoja kikubwa ; Ubinadamu wetu.
Kwahiyo jamii yote ya binadamu inapaswa kumuabudu Mungu. Na kwake yeye kila goti litapigwa na ukweli hautofichika tena. Wakati utafika ukweli utajulikana. Na nuru itaishinda Giza. Na watu watajua njia ya Mungu ndio njia pekee ambayo ni sahihi.