Ramadhani Fupi
New Member
- Jun 29, 2024
- 1
- 0
NURU YA TANZANIA MIAKA KUMI IJAYO SEKTA YA ELIMU
'' Elimu ni ufunguo wa maisha '', huu ni wimbo mkubwa Kwa wanafunzi unaonesha umuhimu wa Elimu katika jamii. Elimu ni ujuzi unaomwezesha mtu yeyote kufanya jambo Kwa ufanisi. Tanzania tumejaaliwa kuwa na vituo mbalimbali vinavyotoa elimu kwa rika tofauti lakini kwa kiasi kikubwa elimu hii imekua na msaada mdogo Kwa watanzania kwasababu haimjengi Mwanafunzi kuweza kuwasilisha mawazo ya darasani katika utendaji hali inayosababisha ongezeko la wimbi la wasio na ajira pamoja na ufanisi mdogo wa majukumu.
Wazee wa zamani pindi mtu alipokosea walikuwa wakisema 'yaliyopita si ndwele tugange yajayo'' wakimaanisha kosa lishatendeka cha msingi ni kutafuta Suluhu la tatizo na kusonga mbele. Hivyo basi, Kufuatia kukua Kwa teknolojia duniani, ninatamani kuiona nchi yangu ya Tanzania katika miaka kumi ijayo mbaka mwaka 2035 iwe imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo katika sekta ya Elimu kama ifuatavyo:
Kwanza kabisa, miaka kumi ijayo natamani kuona kila mwanafunzi anasoma masomo ambayo yatampeleka moja kwa moja kwenye lengo la ndoto yake badala ya mwanafunzi kusoma masomo yote ambayo mengine hayana msingi wowote kutokana na kile anachotaka kukisomea pindi atakapofika elimu ya juu. Hivyo basi kunzia ngazi ya Msingi ni vyema mfumo wa Elimu kupitia walimu utambue lengo la kila mwanafunzi Kisha kila mwanafunzi asome masomo yanayoendana na manatarajio yake. Mfano, kama mtu anatamani kuwa Daktari, anatakiwa asome masomo ya Sayansi tu yatakayomfanya afikie lengo na wala si kusoma kila somo ambayo mengine hayana msingi katika taaluma yake zaidi ya kumuongezea mzigo na upotezaji wa muda.
Tanzania tumekua tukishuhudia watu wengi wakisoma katika ngazi ya elimu ya juu Kwa lengo la kuongeza elimu hasa waajiriwa ambao tayari wapo katika nafasi za kazi, lakini cha kushangaza huyo mtu haonekani hata mara moja darasani zaidi ya kipindi cha mtihani wa mwisho tu, na ikumbukwe kuwa, vyuoni mgawanyo wa alama za mitihani (Marks) umegawanyika mara mbili ambapo Kuna alama za kazi ya darasani (coursework) na alama za mtihani wa mwisho.
Kwa Mfano, Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alama 40 zinatokana na kazi za darasani (coursework) na alama 60 ni za mtihani wa mwisho, Sasa utakuta mtu huyo anaeongeza elimu hahudhurii darasani, je hizo alama 40 huwa anazipataje? na wala husikii kufeli kwake. Hali hii inasababisha kuzalisha watu wasiokuwa na taaluma ya kutosha katika taaluma husika. Hivyo basi, katika miaka kumi ijayo natamani kuwe na sheria inayomtaka yeyote mwenye Lengo la kuongeza elimu aache shughuli zingine Kisha ahudhurie darasani Kwa sababu ya kujifunza kwa ufanisi zaidi lakini kama ana uwezo wa kufanya kazi huku anasoma Kwa wakati huo huo ni Sawa.
Pia, natamani kuondolewa kwa kidato cha tano na Sita badala yake watakofaulu kidato cha nne waendelee na elimu ya chuo kikuu kwasababu ya kupunguza muda unaotumika katika elimu. Hii ni kwasababu Tanzania tumekua tukitumia muda mwingi katika elimu kuliko mambo mengine, hivyo basi katika miaka ijayo nataman kuondolewa Kwa baadhi ya vidato kwasababu hakuna kitu kipya zaidi ya kusoma mambo yale yale. Mfano, wanafunzi wanaosoma masomo ya Sanaa hakuna kitu kipya kati ya 'O level' na wanaosoma 'A Level'
Mbali na hayo, pia baraza la mitihani Tanzania napendekeza litunge mitihani yenye mgawanyo wa namna mbili, nusu ya alama itoke kwenye mtihani unaohusu nadharia na nusu ya pili ni mtihani wa vitendo. Hivyo basi alama za mitihani (marks) ambazo ni 100 kwa kila somo, zigawanywe mara mbili, alama 50 kwaajili ya nadharia na 50 nyingine kwaajili ya kazi ya vitendo (practical) ambapo Mwanafunzi anapsawa kufanya alichojifunza darasani Kwa vitendo wakati huo usimamizi ukiwa wa hali ya juu sawa na usimamizi wa mitihani ya darasani.
Juu ya hayo, pia natamani kuona vituo vya kutolea elimu vya serikali viwe na uwezo sawa na vituo vya watu binafsi Kwa kujenga maktaba za kisasa, maabara za kisasa na walimu wenye uwezo mkubwa katika somo husika. Pia kila Mwalimu awe ametathminiwa katika somo lake na wala siyo Mwalimu mmoja anafundisha masomo matatu peke yake sidhani kama masomo yote atafundisha katika ubora ulio Sawa, jambo hili litawezekana Kwa kuzingatia taaluma ya mtu.
Kwa kumalizia, mafanikio ya kila jambo yanaanza na uongozi bora unaojengwa na nidhamu, Tanzania tunashindwa kupiga hatua ya kimaendeleo katika elimu kwa sababu ya utovu wa nidhamu unaochagizwa na watu wachache. Mfano, baadhi ya walimu kuvujicha mitihani Kwa wanafunzi Kwa lengo la kupata sifa ya kufaulisha wanafunzi wengi ambao bila kufaham watakwenda kutengeneza kizazi tegemezi kama cha Sasa kwasababu ni kawaida kumuona Mwanafunzi aliyehitimu kidato cha nne na asijue kusoma wala kuandika, mwanachuo aliyehitimu shahada ya uandishi wa habari na asijue kuandika habari, kutumia vifaa vya habari wala ujasiri wa kuongea mbele za watu lakini cheti chake kinaonesha ufaulu wa hali ya juu mithili ya Profesa Lipumba msomi mwenye elimu isiyo na mashaka kama kitabu kitukufu cha Qur'an.
Pia ni muhimu Sana miaka ya mbele kila kiongozi aajiriwe kulingana na taaluma yake, Mfano mzuri ni Waziri wa habari, Sayansi na teknolojia ya habari nchini Mh Nape Nauye alisoma uandishi wa habari na sasa ni Waziri wa habari, anafanya vyema kwasababu ndiyo taaluma yake. Lakini mtu aliyesomea ualimu alafu anakabidhiwa uwaziri wa sheria na katiba hatakuwa na ufanisi mzuri kwasababu siyo taaluma yake. Tanzania tunatarajia kufika mbali Sana katika sekta ya elimu, kwa hakika kama tutafika katika hizo hatua ninaamini tutakua taifa lenye nguvu duniani, kwa uwezo wa Mwenyezimungu hakuna kitakachoshindikana.

Upvote
1