Nusu fainali na fainali ya draft

fantastic philip

Senior Member
Joined
Oct 17, 2015
Posts
195
Reaction score
688
Katika michuano ya drafti inayo endelea huko JAVA kitunda sasa ni hatua ya nusu fainali,

NDULI vs DOGO SISCO

DOGO YASINI vs DOGO ASUMANI

Ikumbukwe kua mshindi wa kwanza kujinyakulia laki mbili mshindi wa pili kujinyakulia laki moja na mshindi wa tatu elfu hamsini mechi zinaendelea ASANTENI SANA.



WADAU WA DRAFTI, Mechi ya fainali ndio imeanza kati ya nduli na dogo yasini NDULI Ni huyo mwenye flana NYEUSI DOGO YASINI ni huyo mwenye flana nyeupe, na wakati huo huo kuna mechi inapigwa kati ya DOGO SISCO na DOGO ASUMANI Hii ni mechi ya kumtafuta mshindi wa tatu. ASANTENI.
 
Utatupa mrejesho nani kabeba,

Kwenye hizi za kusukuma kete nlibebaga mbuzi dume huko, Sehemu moja inaitwa Bombambili Songea😅😅😅 huko Tanga hadi mjumbe alitaka kunikabidhi binti kama zawadi

Japo Babu yangu pale Jang'ombe,Zanzibar alinikomaza, kwenye Bao la kete.
 
Duuh huu mchezo sikufanikiwa kuujua vizuri ila napenda sana kuujua.
 
Huu mchezo unachezwa muda huu?

Au kitunda huko ni mchana kwa muda huu?
 
Huu mchezo mbona ushapigwa,Dogo sisco kachapwa 2-0 na nduli
 
WAPENZI WA DRAFTI, Michuano yetu ya kumtafuta mshindi atakaejinyakulia kiasi cha shiringi laki mbili na nusu imefikia tamati hatimae NDULI Ameibuka na ubingwa baada ya kumfunga dogo yasini goli la DHAHABU Michezo ya awali ilimalizika kwa kutoshana nguvu huku kila mmoja akiwa ameingia nyavuni kwa mwenzie mala mbili namaanisha kua katika michezo 14 ya kawaida pamoja na tege 10 NDULI na DOGO YASINI Walitoka sale ya mbili kwa mbili hivyo wakaingia katika kipengere cha goli la dhahabu ambapo iliwekwa sheria ya kufikilia mwisho sekunde 10 tu, katika kipengere hicho NDULI alifanikiwa kupata goli moja zidi ya mpinzani wake jumra ya matokeo yakasoma NDULI 3 vs DOGO YASINI 2 na hatimae nduli akatangazwa kua bingwa, katika mechi nyingine yakugombea nafasi ya 3 DOGO SISCO alimfunga mpinzani wake DOGO HASUMANI goli 3 kwa 0

ZAWADI KWA WASHINDI WETU,

Nafasi ya kwanza NDULI Sh. 250000

Nafasi ya pili DOGO YASINI Sh. 100000

Nafasi ya tatu DOGO SISCO Sh. 50000

Asanteni wote mliokua pamoja nasi katika kufuatiria mtanange huu. [emoji172][emoji172][emoji307][emoji172][emoji172]
 
Hao mnaowaita madogo ni madogo kweli au janja janja? Nataka mmoja wao anifundishe maana kuna kijiwe nacheza kila siku napigwa mimi tu
 
Andika Kiswahili vizuri.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…