shibela
JF-Expert Member
- Jul 3, 2018
- 1,068
- 3,507
Ukimfanyia mtu ubaya, jitenge naye, hata kama anaonekana mpole na mnyonge. Moyo wa mtu ni kama kichaka; huwezi kujua anachoficha.
Hii ni moja ya kumbukumbu mbaya sana maishani mwangu – moja kati ya mbili zilizonikumba.
Kuna mradi niliopanga na Frank, tulipanga vizuri na mipango ikaonekana imekaa sawa. Kosa langu lilikuwa kumuamini Frank na kumwachia yeye awe kiongozi wa mradi huo! Nikatoa akiba yangu yote na kuiweka pale, nikiwa na matumaini makubwa sana.
Miezi miwili tu ikapita, mambo yakaanza kutokuwa sawa na kila siku kulikuwa na kisingizio kipya; mara limeingilia hili, mara limezuka lile! Miezi ilizidi kusonga na taa nyekundu ikawa imewaka kichwani, lakini nikaendelea kujidanganya, sitaki kukubali kama Frank ananidhurumu!
Lakini ukweli ukabainika – Frank kanidhurumu! Nilijaribu kumwambia anirudishie hata nusu ya gharama zangu, lakini akaanza kunizungusha tu, mara anatabasamu kana kwamba hakufanya kosa lolote. Moyo ulikuwa unaniuma sana, nikiwa na stress balaa, hakuna kitu kilichokuwa kinaniendea sawa. Nakiri wazi kuwa hata mapenzi hayajawahi kuniumiza kama dhuruma aliyonifanyia Frank!
Wakati huo, Frank kwake ni kama hakuna kilichotokea; maisha yake yanaendelea vizuri tu.
Nilijikuta nawaza namna gani nitaweza kumkomesha Frank, nikafikiria mpaka kumpa kilema cha maisha ili kila atakapojiona anikumbuke. Lakini hilo wazo lilikataliwa na akili yangu. Sikupenda kushirikisha mtu kwenye hili maana najua hakuna siri ya watu wawili.
Mwisho wa yote, nikajikuta nafikiria kumuua Frank kwa mikono yangu. Hasira ilikuwa imenikamata kiasi kwamba natetemeka, na karibu naanza kuchanganyikiwa. Kila mtu aliyeniuliza kuna nini, nilijikuta nakosa maneno na naishia kulia kwa uchungu. Moyo na akili vilikuwa vimevurugika kabisa, huku mvurugaji anatamba tu mjini kana kwamba hakutenda dhambi.
Nilipanga mpango wangu – nitaondoka nchi bila kuacha alama yoyote, na sitorudi tena mpaka kifo.
Siku hiyo nikampigia simu Frank, nikamwomba tukutane naye akakubali.
Mimi: Una watoto wangapi?
Frank: Hujui nina watoto wangapi? Mbona umeuliza hivyo?
Mimi: Napenda sana watoto. Mimi na Ngosha tunataka kuoana, na ninataka uwe kwenye kamati!
Frank: Sawa, hakuna shida, tutawasiliana!
Hii ilikuwa njia rahisi ya kuhakikisha atakuwa kwenye ratiba yangu.
Nikaomba ruhusa ya muda mfupi kazini na kurudi nyumbani, nikiwa na mpango wa kumuaga mama yangu kabla sijajiharibia maisha yangu.
Nilipofika, mama alinipokea vizuri, akiwa mwenye furaha na kujivunia sana mimi. Tulikuwa tunatembea pamoja kila wakati, na kila tukikutana na mtu lazima ananitambulisha kwa furaha – hata kama hajamuuliza. "Huyu ndiye mwanangu wa mkoa fulani, anafanya kazi fulani!" huku mimi nikiwa sitaki kujulikana kazi yangu hasa ni ipi!
Upendo wa mama yangu ulinifanya nipate utulivu wa fikra, nikawa na amani tena. Nikajiuliza: kwa nini nimuumize mama kwa kwenda jela au kuikimbia nchi kwa jambo kama hili? Pesa zimepotea, lakini nitapata nyingine. Mradi sijapoteza kazi, mikono, au miguu, bado nina nafasi ya kusonga mbele.
Mpaka leo naamini kuwa nilikosa tu ushauri mzuri wakati ule nilipodhurumiwa, na ndio sababu nilifikia mawazo ya mbali.