Nyabibwe: Mikononi mwa M23

Nyabibwe: Mikononi mwa M23

MBOKA NA NGAI

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2025
Posts
350
Reaction score
576
Wakati nchi ya Malawi ikiamua kuondoa majeshi yake nchini Congo, kwa mission ya SAMIRDC, ya nchi a SADC;
Na baada ya tangazo la M23, la kusitisha mapigano, mpaka sasa, mji wa Nyamibwe, tayari umeangukia mikononi mwa M23.

Mashambulizi yameanza mapema leo, na ndo yameacha mji huo uliopo kilomita chache kuelekea uwanja wa ndege wa Kavumu ukiwa mikononi mwa M23. Siku za nyuma, umoja wa mataifa na serikali waliondoa wafanyakazi wao mjini humo kuhofia usalama wao.

Akizingumzia tangazo la kusitisha mapigano la kundi la M23, waziri wa mambo ya nje Therese Kaikwamba Wagner, alisema hana imani na tangazo hilo, maana siku zote M23 imekuwa ikitangaza hivo na mapigano yakaendelea. Msemaji wa M23 alipotafutwa, amesema yuko bize hatoweza kuongelea jambo hilo.

Nyabibwe, ni mji uliopo km 70 kutoka Bukavu, na km 30 kutoka uwanja wa ndege wa Kavumu.


Source: businesslive.co.za, washingtonpost, abc news
 
Back
Top Bottom