Nyakati hizi ni kati ya saa ngapi na saa ngapi?

Ustaadh

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2009
Posts
413
Reaction score
19
Kwa wanaofahamu naomba mnijuze ALFAJIRI, ASUBUHI, MCHANA, ALASIRI, JIONI, USIKU, USIKU WA MANANE ni kuanzia saa ngapi hadi saa ngapi?
 
mi najua matukio kulingana na hayo maneno ila muda hata mimi unanisumbua........eg usiku wa manane - wkt wa kukata nyavu madirishani mwa watu....
 
Kwa wanaofahamu naomba mnijuze ALFAJIRI, ASUBUHI, MCHANA, ALASIRI, JIONI, USIKU, USIKU WA MANANE ni kuanzia saa ngapi hadi saa ngapi?
Kwa mpangilio kadri ya ulivyouliza ni saa 10-11 alfajiri,12-5 asubuh,6-8 mchana,9 adhuhuri,10alasiri,11-01jioni,02-05 usiku,06-09usiku wa manane.
Saa ziko Kiswahili!
 
Mpangilio uko hivi~ Saa 10-11 Alfajiri, 12-3 Asubuhi, 4-5 Adhuhuri, 6-8 Mchana, 9-10 Alasiri, 11-1 Jioni,
2-6 Usiku, 7-9 Usiku wa Manane. NI SAA ZA KISWAHILI,
Hii usiku wa manane, kwa mtazamo wangu inachukuliwa kama kivumishi cha usiku mzito yaani zaidi ya saa sita.
Lakini kawaida kuanzia saa mbili hadi saa tisa ni usiku.

Tusubiri wataalamu wenyewe waje.
 
Saa 10-12 ALFAJIRI,Saa 1-5 ASUBUHI,Saa 6-8 MCHANA,Saa 9-10 ALASIRI,Saa 11-1 JIONI,Saa 2-6 USIKU 8-9 USIKU WA MANANE
 
Mbona mnanichanganya sasa wadau
Kwa mpangilio kadri ya ulivyouliza ni saa 10-11 alfajiri,12-5 asubuh,6-8 mchana,9 adhuhuri,10alasiri,11-01jioni,02-05 usiku,06-09usiku wa manane.
Saa ziko Kiswahili!

Saa 10-12 ALFAJIRI,Saa 1-5 ASUBUHI,Saa 6-8 MCHANA,Saa 9-10 ALASIRI,Saa 11-1 JIONI,Saa 2-6 USIKU 8-9 USIKU WA MANANE
 
Adhuhuri sio jioni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…