Nyakati za sasa zinahitaji uwe na rafiki wa faida na sio rafiki wa kupiga porojo

Nyakati za sasa zinahitaji uwe na rafiki wa faida na sio rafiki wa kupiga porojo

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Nyakati zimebadilika; nyakati za sasa zinahitaji uwe na rafiki wa faida na sio rafiki wa kupiga tararila (maneno maneno).

Pia tukumbuke, maisha yanahitaji pesa na sio maneno.

Kwa mazingira hayo, ni vizuri kutafuta rafiki wa faida; ambaye uwepo wake unakuwa una tija. Unaweza kutumia majukwaa mbali mbali, kupata hao marafiki.

Kwa mfano; unataka marafiki angalau wenye mitaji ya kuanzia laki tano, na wawe wanapatikana mikoa au nchi tofauti tofauti; unaweza kuanza hivi:-
  • Utatoa tangazo la kutafuta rafiki wa kibiashara mwenye mtaji wa kuanzia laki tano, awe anapatikana katika mikoa au nchi kadhaa.
  • Kila atakayepatikana aeleze bidhaa zinazopatika na zinazohitajika kwa wingi sehemu aliyopo.
  • Baada ya hapo, jibatizeni majina, wewe mwenye wazo jiite D1 (Director 1), na hao wengine wajiite D2, D3, D4....Dn (Mtajiita 'Director') kwa sababu siku zinavyozidi kwenda, kila mmoja atakuwa na timu au ofisi yake.
  • Chukua bidhaa zinazopatikana kwa wingi kwako na kuzisafirisha zinapohitajika kwa D2, D3,....Dn, na wao wafanye hivyo hivyo kukutumia zile zinazohitajika kwako.
  • Fanya mauzo, na maisha yaendelee.
Karibuni kwa mjadala.
 
Back
Top Bottom