Nyama choma festival: Ndio watanzania tunaloliweza tu

Andrew123

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2012
Posts
8,358
Reaction score
10,976
Watanzania tunasifika duniani kwa kupenda vitu vya kula kula na kunywa kazi HAPANA yaani ukitaka kujua wa TZ tunavyopenda hayo nenda kwenye vikao vya harusi watu wanavyolumbana kuhusu aina ya msosi na idadi na aina ya vinywaji Ukute hapo hata mwanae kakosa ada ya kwenda shule.
 

kwani wanaokwenda kwenye vikao vya harusi na hizo nyama choma festival siyo wafanyakazi
 
Zinasaidia kutoa ajira. Kuna ng'ombe watauzika, wabebaji toka machinjioni watalipwa, wauza nyama buchani watapata faida, wauza mkaa watauza, viungo vitauzika, vijana wa kupika watapata pesa, aliyechukua dili atalipwa, na faida nyingine nyingi za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni
 
Hata hueleweki. kwani wanakula bila kulipa?

Na kama wanalipa ina maana wanafanya kazi .
 
Hizo ni desturi zetu, mataifa yote yanafanya harusi kutokana na mila na desturi zao. we kama huna hela usichange ni siku ikifika ya nyumbani kwako usichangishe watu. Maisha sio kazi tu, furaha, chereko chereko na kujichanganya na jamii pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…