Nyama choma yenye asali

Nyama choma yenye asali

Profesa

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Posts
905
Reaction score
624
Nimejaribu hii na nimegundua hubadilisha ladha kabisa ya nyama. Unaweza kuongeza vioungo vingine kadri unavyopenda ila mimi hupendelea kuichanganya nyama na vinega au limao, chumvi na tangawizi. Unaifunika nyama yako na nilon wrap kwa dakika ishirini ndani ya friji, inaweza pia kulala usiku mzima kuhakikisha viungo vinaingia ndani vema. Asali yako unaiweka wakati nyama inapokaribia kuiva hii huifanya iwe na ladha ya kipekeee na rangi ya kuvutia ya brown nzuri.

Choma nyama kwa moto wa wastani, kama unatumia jiko la kuchomea, basi koleza mkaa mpaka ukolee kabisaa then ufunike na majivu. Mimi hupendelea zana rahisi, nimechimba shimo la futi mbili kwa futi moja na nusu na nimenunua wavu wa square kwa ajili ya kuokea nyama. Shimo hilo lina urefu wa robo tatu ya futi. Unaweza kuweka vitofali pembeni ili wavu usishike udongo. Shimo hilo mimi hupendelea kulifunika kwa aliminium foil ili kutunza joto.

Koleza moto pembeni na kisha ukisha kolea uweke kwenye shimo lako. Weka wavu juu, hakikisha wavu wako umeupaka mafuta kidogo ili nyama isishike. Weka nyama juu na uifunike kwa foil kutunza joto. Iache kwa dakika kama 30-40 ndipo uichungulie. Geuza kama upande mmoja umebadilika rangi na endelea kugeuza mpaka uridhike kuwa nyama yako imeiva kwa kiwango cha kuridhisha. Angalia moto usiwe mkali sana hasa hatua za mwanzo, ukiwa mkali weka majivu juu kidogo. Wakati mwingine hupendelea kuweka kibakuli cha bati chenye maji yenye viungo na chumvi (kama unatumia chumvi) chini kwenye moto ili nyama iwe na ulaini na mvuke wake kuifanya isiwe kavu (si lazima sana kama utakuwa unaipaka nyama yako maji yenye asali na viungo ili isikauke wakati unaigeuza).

Katika hatua za mwisho si vibaya moto ukiwa mkali zaidi kidogo ili kuweka ule ubrown unaoutaka. wakati mwingine nyama huiva kwa mvuke bila kubadilika sana rangi kutegemea na jinsi ulivyotunza kwa kufunika wakati wa kuchome.

Hapa china ni picha ya baadhi ya nyama ambazo nilichoma mojawapo ya wikiend hasa siku za Jumapili.
 
Attachments

  • DSC01356.JPG
    DSC01356.JPG
    1.7 MB · Views: 477
Mkuu,
Dah hii ningeipata last wiki mbona ingekuwa balaa. Lakini sijachelewa, na naamini taste yake ni chiboko. Mimi hutumia apple cider vinegar kuchemshia nyama na ukiiunga chuzi lake na taste ni tamu sana hasa ukiweka nazi na swaumu pia na vikorombwezo vingine ...

Sasa hii wiki ijayo lazima nifanye mavitu haya, kwanza kwa kuanzia nitajaribu nyama ya mbusi.. Tena unajua vinega na ndimu/limau vinasadia sana kutoa mafuta yote ktk nyama huku vikiacha nyama fresh na laini (hata uchemshe ng'ombe aliyeandamana mtwara au jogoo aliyekula mataruma ya reli ya kati, hii mchanganyiko sio mchezo nyama lazima ilainike..
 
Thanx kwa kuturithisha utaalamu!
 
sku nyingine jaribu kuchemshia bia ya serengeti utanipa majibu!
 
Back
Top Bottom