Nyama ya ng'ombe ya foil

Yerusalem

Member
Joined
Oct 5, 2011
Posts
71
Reaction score
72
Wanajukwaa naomba kujuzwa jinsi yakuandaa pishi hili nalipenda sana
Cc farkina
 
Halina ufundi kivile hasa kama una slow cooker au oven
Chukua nyama uindae na kuikatakata kwa vipande vya kawaida isiwe nyingi sana kilo moja au nusu hivi
Iweke kwenye foil paper pamoja na viungo vilivyokatwa tayari kama kitunguu saumu na maji tangawizi hoho karoti chumvi na pilipili kwa mbaali
Funga vizuri na foil paper kisha oka au banika kwenye oven yako au slow cooker , muda ni dk 60 mpaka 90
 
Ha ha ha kiswahili lugha ngumu ila nashukuru wapo walioelewa, ahsante kwa kunirekebisha
 
Duh Mshana Jr miaka mitano leo ndio nafunguka kuwa kuna utaalam wa kutumia foil kweny kuoka nyama
nina sherehe keshokutwa nataka wageni wale kwa foil tu sina mafuta ya kukaangia hizo nyama
MSAADA
katika mchanganyiko huo naweza kuweka na viazi mviringo? au mpaka nivichemshe
nataka viwe ndani ya mchanganyiko huo kwa kila foil
 
Ooh OK OK...!!! Unaweza pia kuvioka direct bila kuchemsha kwanza

Jr[emoji769]
 
Ooh OK OK...!!! Unaweza pia kuvioka direct bila kuchemsha kwanza
Jr[emoji769]
Mkuu nimefanya hivyo kwa kuweka viazi na nyama ya ngome km 1kg nika,alizia na kapapai
ni tamu laini karibu mezani
 
samahani kama ulitumia oven uliweka moto kiasi gani?
niliweka full (kati ya nyuzi 150 na 180 kwa muda wa dk 60 nilipofungua foil nilikuta imeiva hivyo nikaongeza dk 15
(yaani unakuta nyama imeiva laini kabisa na kamchuzi kake) unaweza kuongeza muda ili ikauke
 
asante ntaijaribu hii sikukuu za hivi karibuni.pia nimeona umetaja papai je linafaa lipi lilioiva sana au kawaida?
 
asante ntaijaribu hii sikukuu za hivi karibuni.pia nimeona umetaja papai je linafaa lipi lilioiva sana au kawaida?
zaidi papai lililoiva unakata kipande kidogo tu km unachota vijiko 2 vya chakula halafu unaikorogea hiyo nyama na ile michanganyiko ya kitunguu saumu Tangawizi na chumvi kidogo ukipenda pilipili
Papai likizidi unaweza kuta nyama imegeuka au nyambulika hata kibogoyo akala
 
asante sana 😊😊
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…