Elections 2010 Nyambari Chacha Nyangwine Kurudisha Tarime CCM..Hongera NEC Kwa Kusoma Alama Nyakati

Ngurudoto

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2008
Posts
208
Reaction score
26
Tangu jimbo la Tarime kubebwa na Marehemu Chacha Wangwe(CHADEMA), na makundi mawili yaliyokila Chama cha Mapinduzi Tarime, imekua vigumu kwa CCM kurudisha jimbo hilo, hata Uchaguzi mdogo ukapita ukamleta Mhe. Charles Mwera-CHADEMA (ambae sasa kakimbilia CUF) pale ,ila uteuzi wa Mwanasiasa kijana mahiri, msomi na mwandishi (miaka 34), Mhe. Nyambari Chacha Nyangwine hakika ni matumaini na tegemeo kulirudisha nyumbani jimbo la Tarime ambalo kusema kweli limerudi nyuma sana na mpaka kuwa kanda maalum ya kipolisi kutokana na uhalifu uliokithiri, pamoja na kwamba kuna na wanaCCM wengi zaidi 30,000 jimboni.

Hakika ninaipa pongezi za dhati Halmashauri kuu ya CCM (NEC) kusoma alama za nyakati, kutomleta tena Mhe. Kangoye aliyeangushwa na Mwera na kuleta mzungumzaji mzuri kijana, kampeni ya vijana kati ya kada huyu kijana Nyangwine na mgombea kijana wa CHADEMA yaani Waitara itakuwa burudani ya kidemokrasia na kwa ndugu zangu wanaoelewa siasa za Tarime, Kule bila NGUVU,Nguvu ya hoja na ukakamavu: huwezi kuwa Mbunge wa jimbo hilo ndani ya kanda maalum ya kipolisi ukiwa lelemama..Hushindi bila kuwa tafu Na fizikali fiti..

Mwaka huu ni Tarime Vijana: Nyangwine (CCM) vs Waitara (CHADEMA) & Mwera(CUF)...tusubiri raundi 12 za kampeni, ila upepo wakati huu naona kama unaelekea zaidi CCM..Mnasemaje JF?
 
Si unajua hapa JF huwa hatushughuliki na kampeini, tunashughulika na ukweli.
Ebu tuletee facts kuhusu Nyangwine tuzione isije kuwa tunashughulika na kihiyo hapa, maana NEC/CCM safari hii wameamua kuvunja rekodi. Wana wagombea wa darasa la saba 37, na 123 wa form four. Jamani hili si tusi, naonyesha jinsi hali ilivyo. Wa kujiendeleza bado naendelea kuhesabu.
 
Hilo la viwango vya elimu hasa msingi na sekondari imenishtua sana,

Hasa wengi wana majina ya kiislamu, hii huonyesha nini.

Malaria Sugu nisaidie kulijibu hili.
 
:welcome:nikiwa kama mdau wa siasa za tarime kwa mtazamo wangu nyambari nyangwine hana uwezo wa kupambana na mwikwabe mwita kwa sababu zifuatazo
1.uwezo wa kujieleza na kuunda hoja ni mdogo kulinganisha na mwita ambaye alijijengea heshima tangu akiwa raisi daruso
2.nyambari hana uwezo wa kubishana na wakubwa ikumbukwe mwita mwikwabe aliteuliwa kuwa katibu wa nchimbi lakini alijibu kuwa hawezi kwenda kupika chai ofisini kwa mwanaume mwingine kwa wakurya hii ni kuonesha uanaume
3.nyambari na mwita wote wanatoka katika koo moja ya wairegi hivyo nafasi yake ya kushawishi koo nyingine ni ndogo ukilinganisha na mwita
4.umaarufu na nguvu ya chadema tarime ni kubwa kwani mtaji wa chadema ni vijana
 
Mhe. Nyambari Chacha Nyangwine hakika ni matumaini na tegemeo kulirudisha nyumbani jimbo la Tarime ambalo kusema kweli limerudi nyuma sana na mpaka kuwa kanda maalum ya kipolisi kutokana na uhalifu uliokithiri, pamoja na kwamba kuna na wanaCCM wengi zaidi 30,000 jimboni

Nani kalirudisha nyuma kama siyo serikali ya CCM
 
Mwita Ke, unaelewa kuwa vijana watagawanyika sababu wote ni koo ya Wairegi na wote Nyangwine na Mwikwabe Waitara ni vijana..Rasilimali ya vijana haiko upande wowote CCM au CHADEMA watagawana.
Uchaguzi mdogo,vijana walikataza wake zao kupiga kura sababu wanawake wengi ni CCM, safari hii inaweza kutokuwa hivyo..Alafu Hapo sababu ya ukoo (wote wairegi) itakuwa inapunguza nguvu kwa CHADEMA au kugawana kura na Nyangwine.

Pili,Wazee wairegi, kwa wakurya wanajua, tamko la wazee ni muhimu katika jamii hizo, baada ya Nyangwine kupitishwa, wazee wametamka hawataki Upinzani na kumsupport Nyangwine.

Tatu: factor ya Charles Mwera kumega nguvu ya mwikwabe Waitara..Makundi ndani ya Chadema baada ya Mhe. Mwera kukosa na kuhamia CUF

Nne nayo: Nguvu ya Dola Chacha Nyangwine Bofya hapa..<http://www.radiofreeafricatz.com/vitabu-Tarime.html>...Wapiga kura wanapenda takrima
 
wizi wa ng'ombe
 
wapinzani wanatuangusha sana Tanzania
 
Ni kweli kuwa wanawake wengi ni CCM? Wanawake wanachangia kiasi gani kupiga kura ukilinganisha na wanaume?
 
:welcome:nikiwa kama mdau wa siasa za tarime kwa mtazamo wangu nyambari nyangwine hana uwezo wa kupambana na mwikwabe mwita kwa sababu zifuatazo
1.uwezo wa kujieleza na kuunda hoja ni mdogo kulinganisha na mwita ambaye alijijengea heshima tangu akiwa raisi daruso
2.nyambari hana uwezo wa kubishana na wakubwa ikumbukwe mwita mwikwabe aliteuliwa kuwa katibu wa nchimbi lakini alijibu kuwa hawezi kwenda kupika chai ofisini kwa mwanaume mwingine kwa wakurya hii ni kuonesha uanaume
3.nyambari na mwita wote wanatoka katika koo moja ya wairegi hivyo nafasi yake ya kushawishi koo nyingine ni ndogo ukilinganisha na mwita
4.umaarufu na nguvu ya chadema tarime ni kubwa kwani mtaji wa chadema ni vijana
Mwita hapo umenena yaliyosahihi kabisa baina ya watu hao wawili nadhan hata mtoa mada amekuelewa ila analeta ubishani tu..Niliwahi kuishi kwnye kijiji cha Nyangoto kwa kweli Chadema wananguvu sana katika wilaya nzima ya tarime..nachokiona sasa kutakuwa na ushindani kwa hao wawili waitara na Nyambari ila huyu mwera nadhan atapata kura za kutoka kwa familia yake..ameonesha anauchu wa madaraka kwa kukihama chama kisa kakosa nafasi!...I bet Chadema watachukua tena jimbo lao
 
Hivi huyu bwana Nyambari ameshabadilika na kujikosa na Ufisadi? Siye huyu aliyeshawishi mitaala ya elimu tanzania ibadilike ili aweze kuuza vitabu vyake kwa maslahi yake hata bila kujali ushindani kimataifa dhidi ya kinachopatikana katika vitabu vyake??
 
sorry, kujikosha

Edit Post Reply Reply With Quote Thanks
Next time apply hiyo bolded hapo juu unapoona kuna makosa kuna makosa kwenye post uliyoituma
...Ni kweli ndio huyo huyo mjasiriliamali ambae aliaanza kazi hiyo mda mrefu akiwa anasoma nakufundisha watoto wa St. Mary
 
Hivi huyu bwana Nyambari ameshabadilika na kujikosa na Ufisadi? Siye huyu aliyeshawishi mitaala ya elimu tanzania ibadilike ili aweze kuuza vitabu vyake kwa maslahi yake hata bila kujali ushindani kimataifa dhidi ya kinachopatikana katika vitabu vyake??

Nyangwine ni bonge la fisadi
 
Mwita Ke, unaelewa kuwa vijana watagawanyika sababu wote ni koo ya Wairegi na wote Nyangwine na Mwikwabe Waitara ni vijana..Rasilimali ya vijana haiko upande wowote CCM au CHADEMA watagawana.
Uchaguzi mdogo,vijana walikataza wake zao kupiga kura sababu wanawake wengi ni CCM, safari hii inaweza kutokuwa hivyo..Alafu Hapo sababu ya ukoo (wote wairegi) itakuwa inapunguza nguvu kwa CHADEMA au kugawana kura na Nyangwine.

Pili,Wazee wairegi, kwa wakurya wanajua, tamko la wazee ni muhimu katika jamii hizo, baada ya Nyangwine kupitishwa, wazee wametamka hawataki Upinzani na kumsupport Nyangwine.

Tatu: factor ya Charles Mwera kumega nguvu ya mwikwabe Waitara..Makundi ndani ya Chadema baada ya Mhe. Mwera kukosa na kuhamia CUF

Nne nayo: Nguvu ya Dola Chacha Nyangwine Bofya hapa..<http://www.radiofreeafricatz.com/vitabu-Tarime.html>...Wapiga kura wanapenda takrima

Kama haya ndiyo Nyangwine ataenda kusema bungeni - ukabila na ujinsia, basi this guy is crazier than Makamba.

Pumba juu ya pumba.
 
Hilo la viwango vya elimu hasa msingi na sekondari imenishtua sana,

Hasa wengi wana majina ya kiislamu, hii huonyesha nini.

Malaria Sugu nisaidie kulijibu hili.
Acha udini ndugu badilika na uwe muungwana,post 125 tuu tayari unaendekeza siasa za chadema udini udini udini!Utakupeleka wapi,badilika!
 
ha ha ha ... siasa za chadema za udini? bwa ha ha ha ha.

Na hili linatoka kwa msemaji wa vuguvugu la mahakama na haki za kiislam Tanzania?
 
Back
Top Bottom