minda
JF-Expert Member
- Oct 2, 2009
- 1,068
- 67
wakuu wengi mliosoma elimu ya upili (na hata msingi) miaka ya hivi karibuni mtakubaliana nami kwamba huyu jamaa, nyambari nyangwine, ni miongoni mwa ma-celebrity wa nji hii.
huyu jamaa kupitia stationery yake amefanikiwa kutoa vitabu vya summary kwa masomo tofauti kwa mtindo wa vijitabu na maswali na majibu na amesaidia walimu na wanafunzi wengi kurahisisha zoezi la kusoma nk
ukweli kuhusu celebrity huyu ni kwamba amepitishwa na chama tawala kukiwakilisha kwa ngazi ya ubunge kupitia jimbo la uchaguzi la tarime.
baada ya kula sana kupitia daraja-bua la elimu ya bongo (a.k.a Questions & Answers), nina wivu sana kuona kwamba jamaa atakuwa na uwezekano wa kula tena keki ya uhakika kupitia mjengoni; tena safari hii sio keki ya wanunua vitabu bali keki ya taifa- jasho la mlipa kodi wa nji hii.
namtakia kila la heri katika safari yake hii ya kihistoria mungu amtangulie kama atakavyowatangulia wagombea wa vyama vingine (simpigii kampeni).
walimu wavivu watamkumbuka sana huyu jamaa kwani amewasaidia kuandaa masomo yao; wanafunzi wavivu wa kuhudhuria vipindi watamlilia pia kwani vitabu vyake ndio hivyo hivyo vinavyotumiwa na walimu wao kwa kufundishia bila kubadili hata neno moja, kiasi kwamba mwanafunzi akihudhuria au asipohudhuria vipindi, yote sawa...
au mnasemaje wakuu?