Mtu akithubutu kuwapora ushindi watu hawa anatafuta Matatizo.
Nakuomba umsome vizuri Masauni, umwelewe vizuri.
Mkuu 'Erythro', hivi kwa nini siku hizi hatuelewani vizuri? Nadhani umekuwa na maneno mengi zaidi kiasi kwamba unaanza kupoteza umakini bila kujitambua mwenyewe.
Masauni anahimiza wajumbe wake huko mitaani, wa nyumba kumi wafanye kazi yao, wewe hapa unatazama tu umati wa watu ambao hawakupewa mkakati wowote halafu unapandwa mori kichwani!
hawa watu wanahitaji maelekezo, elimu ya kuzuia kura zao zisiharibiwe. Kuja kwao hapa ni kutafuta njia hizo, lakini hasahasa huko wanakotokea mitaani kwao.
Masauni anakwambia, yeye ndiye mmilki wa "mapolisi", kama alivyo wataja mwenyewe na anawajaza upepo machawa (akina Lucas) wawadhibiti nyinyi huku mitandaoni!
Kama watu wanaojielewa, kama msomi Kibatala nao wanaanza kulia kwa kushindwa kujuwa wafanye nini kutokana na jinsi CCM ilivyotanda na kuziba kila sehemu...; halafu CHADEMA isiweze kuona hali hii ngumu na kujitahidi kutafuta njia za kupambana nayo, waTanzania wapeleke wapi matumaini yao sasa?
Wasubiri muujiza wa Gen Z hapa kunyanyuka kama uyoga, bila ya maandalizi yoyote? Mbona hawa Gen Z ya hapa nao ni mateka wa CCM kama sisi wengine wote? Chawa huwaoni wametanda kila mahali?