ILIKUWA ni ya mwaka pale nyani aliyepanda juu ya mti kama vile anataka kuona na kusikia vizuri zaidi alipomkojolea Rais Banda (mpya) wa Malawi pale Ikulu, Lusaka.
Rais huyo alikuwa akizungumza na waandishi wa habari na kutokana na hali ya hewa kuwa nzuri siku hiyo aliamua wakae bustanini nje, chini ya mti aliokuja kuukwea nyani huyo ambaye ni mmoja wa wakazi wa bustani ya Ikulu.
Rais alipokojolewa alikuwa akidhalilisha demokrasia na upinzani na kumshambulia moja kwa moja mpinzani wake mkuu, Bw. Sarta.
Baada ya kujifuta mikojo ya nyani huyo Rais huyo alisikika akiahidi kuwa atamzawadiwa Sarta nyani huyo.
Pamoja na yeye kusema kwamba mkojo huu ni ishara ya neema na baraka zitakazofuata baadaye wengi wanaamini nyani huyo amesaidia kuwakumbusha viongozi wetu kuwa wasidharau upinzani na dharau yao inaweza ikatuumiza wengi.
Bw. Sarta hakupatikana na waandishi hao ili atoe maoni yake kuhusu oga ya mwaka ya Rais Banda. Hatuelewi kama mwandishi wa BBC huko Lusaka aliweza kupata picha ya muogo huo au la. Pengine kina Ngahyoma na Majura kwa kutumia intercom na Zambia wanaweza kutupasha zaidi.
Habari hizi zipo mtandaoni kwenye website ya Network Afrika asubuhi ya leo.
Kuwa na subira maana inaelekea kila mtu duniani anataka kuisoma habari hiyo na inachukua muda kushuka na kufunguka.