Nyani amkojolea Rais

Iga

Senior Member
Joined
Dec 17, 2007
Posts
112
Reaction score
6
ILIKUWA ni ya mwaka pale nyani aliyepanda juu ya mti kama vile anataka kuona na kusikia vizuri zaidi alipomkojolea Rais Banda (mpya) wa Malawi pale Ikulu, Lusaka.

Rais huyo alikuwa akizungumza na waandishi wa habari na kutokana na hali ya hewa kuwa nzuri siku hiyo aliamua wakae bustanini nje, chini ya mti aliokuja kuukwea nyani huyo ambaye ni mmoja wa wakazi wa bustani ya Ikulu.

Rais alipokojolewa alikuwa akidhalilisha demokrasia na upinzani na kumshambulia moja kwa moja mpinzani wake mkuu, Bw. Sarta.

Baada ya kujifuta mikojo ya nyani huyo Rais huyo alisikika akiahidi kuwa atamzawadiwa Sarta nyani huyo.

Pamoja na yeye kusema kwamba mkojo huu ni ishara ya neema na baraka zitakazofuata baadaye wengi wanaamini nyani huyo amesaidia kuwakumbusha viongozi wetu kuwa wasidharau upinzani na dharau yao inaweza ikatuumiza wengi.

Bw. Sarta hakupatikana na waandishi hao ili atoe maoni yake kuhusu oga ya mwaka ya Rais Banda. Hatuelewi kama mwandishi wa BBC huko Lusaka aliweza kupata picha ya muogo huo au la. Pengine kina Ngahyoma na Majura kwa kutumia intercom na Zambia wanaweza kutupasha zaidi.

Habari hizi zipo mtandaoni kwenye website ya Network Afrika asubuhi ya leo.
Kuwa na subira maana inaelekea kila mtu duniani anataka kuisoma habari hiyo na inachukua muda kushuka na kufunguka.
 
kwa kweli nimecheka sana nilipoiona sky leo asubuhi, rais alikuwa anaongea kwa nyumba akatokea huyo nyani akamgusa rais jamaa akastuka alipomuona kama ni nyani akaanza kucheka kutoa comment kuhusu huyo nyani, nyani akapanda juu ya mti wakati rais anaendelea kucheka akashusha hivyo vitu ni balaa.
 
Ahhahaha hajawazoeaa waliotangulia wameshawazoea...yeye ni mgeni nyani hawamjuiii
 
ILIKUWA ni ya mwaka pale nyani aliyepanda juu ya mti kama vile anataka kuona na kusikia vizuri zaidi alipomkojolea Rais Banda (mpya) wa Malawi pale Ikulu, Lusaka.

Ili kuweka kumbukumbu vizuri Banda ni rais wa Zambia na si Malawi.
 
Angemkojolea Mtu kama Obama akione cha mtema kuni. Jamaa asingemkawiza kama alivyomwdhibu yule inzi..

LOL!
 
Mwanaume yeyote kukujolewa ni soo, kwanza unaruhusu vipi kukojolewa?
Ulitaka amuombe ruhusa nyani ili (rais) akojolewe? Wewe ukipita road kunguru akakuchafua, huwa unakuwa umemuomba ruhusa?
 
Niliposoma mara ya kwanza nilihisi labda ni yule member wa JF mwenye Jina la Nyani Ngabu...ala kumbe ni Nyani Mnyama pet wa Ikulu kwi kwi kwi
 
Ulitaka amuombe ruhusa nyani ili (rais) akojolewe? Wewe ukipita road kunguru akakuchafua, huwa unakuwa umemuomba ruhusa?

wewe sinkala vipi, kwa hiyo wewe kukojolewa unachukulia poa tu? du hata kuchafuliwa pia hujali?
 
Mwanaume yeyote kukujolewa ni soo, kwanza unaruhusu vipi kukojolewa?

Mbona mwenzako kakojolewa na kanyamaza Bwana? Ungekuwa wewe uliyekojolewa, ina maana ungejiua?
 
Hi ni ajali tu iliyompata rais banda kama zilivyo ajali zingine zozote hakuna cha ajabu hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…